(+Video)Kwa sasa niko 'single' sina mpenzi,'msanii Nicha the Queen asema
- Nicah the Queen asema hana mpenzi yuko 'single' huku akisema atarejea kwenye tasnia ya muziki
Msanii Nicah the Queen akiwa katika mahojiano na radiojambo aliweka mambo wazi na kusema kwamba mchekeshaji Ofweneke ni baba mzuri sana licha ya wao kutengana.
Huku akizungumzia umaarufu wake Nicha alisema, kuwa baba wa watoto wake hakufanya afahamike mitandaoni.
"Ofweneke hakufanya nifahamike sana kwenye mitandao ya kijamii, amekuwa baba mzuri kwa watoto wangu
Niliachana na aliyekuwa mpenzi wangu kwa ajili tulikuwa mbali, sana sana hangeelewa kamba mimi ni mama ananiita tunaenda kujivinjari lakini wakati huyo mimi nawasaidia watoto wangu kufanya kazi ya ziada
Kwa sasa sioni mtu niko single lakini akija ni sawa asipokuja tunangoja kutoka kwa Mungu," Alisema Nicah.
Nicah alifichua kwamba mwaka huu atarejea kwenye tasnia ya muziki.
"Sikuwa nimeacha muziki lakini nitarejea mwaka huu, baada ya uhusiano wangu kukamilika nilikuwa napitia mambo mengi sana
Kama mwanamke kuwa katika tasnia ya burudani si rahisi sana,"
Hii hapa video ya mahojiano yote;
The video could not be loaded.