In Summary
  • Harmonize achorwa tattoo ya uso wa hayati Magufuli kwenye mguu wake
  • Msanii wa bongo Harmonize ni msanii ambaye amekuwa akikejeliwa sana mitandaoni kwa ajili ya vitendo vyake

Msanii wa bongo Harmonize ni msanii ambaye amekuwa akikejeliwa sana mitandaoni kwa ajili ya vitendo vyake.

Siku chache zilizopita alitoa kibao huku akimshirikisha Awilo Longomba huku akivunja rekodi ya staa wa bongo Diamond.

KUpitia kwenye mitandao ya instagram Harmonize alipakia video akichorwa mchoro wa tattoo wa uso wake hayati John Pombe Magufuli.

 

Baadaye alipakia picha huku mashabiki wakitoa hisia tofauti.

KUlingana na Harmonize aliamua kuchora uso wake mwendazake Magufuli ili kumuomboleza na kumkumbuka.

Kwenye tattoo yake aliandika maneno haya;

"Mimi nime sacrifice Maisha yangu Kwaajili ya Watu Maskini”. R.I.P KAMANDA," ujumbe ulisoma.

Kulingana na mashabiki wengi ni kuwa msanii huyo anapenda sifa na kiki nyingi katika maisha yake.

Maoni yako ni yapi kuhusu tattoo yake Harmonize je amefanya jambo nzuri au ni sifa tu anatafuta?

 

View Comments