'Kazi ya mikono yangu itabarikiwa milele,' Kate Actress azungumza baada ya kutoa kibao kipya na msanii Mr Seed
- Muigizaji Catherine Kamau almaarufu Kate Actress ni mmoja wa wanawake mashuhuri ambao wamebarikiwa na talanta tofauti
- Kibao hicho kinazungumzia jinsi mapenzi yanapaswa kuwa kati ya wapenzi wawili, huku wakifunga ndoa
Muigizaji Catherine Kamau almaarufu Kate Actress ni mmoja wa wanawake mashuhuri ambao wamebarikiwa na talanta tofauti.
Kate amewashangaza mashabiki wake baada ya kutoa kibao kinacho fahamika kama 'Ndoa' akimshirikisha msanii Mr Seed.
Kibao hicho kinazungumzia jinsi mapenzi yanapaswa kuwa kati ya wapenzi wawili, huku wapenzi hao wakifunga ndoa.
Kate amejiunga na wanawake kama Avril,Vivian, Nadia MUkami miongoni wa wengine ambao wamo katika tasnia ya burudani na wanafanya vyema katika kazi yao ya usanii.
Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram Kate alisema kwamba kazi ya mikono yake itabarikiwa milele.
Pia alimshukuru msanii Seed kwa kumualika na kufanya kazi pamoja.
"Nimekaa hapa na inhaler pris👀 .'Kazi ya mikono yangu itabarikiwa milele @mrseedofficial kwa kupiga simu hiyo, nilifurahi kufanya haya," Kate alinakili.
Mashabiki walimpongeza Kate kwa hatua yake na hizi hapa baadhi ya jumbe zao;
celestinegachuhi: Booobooo😍😍🔥🔥I loved your work
kanyiri_marangu: Sasa tunangoja collabo yako na samidoh
mercy_wakiyo: A BANGER!!!!!! deffinately playing this at my wedding inshallah!!
queen.nabilah: You sound soooo Good ! you should be doing it often!! 🔥🔥
margie.jewel: 🔥🔥🔥🔥🔥🔥 it's fire fire fire
Hii hapa video ya kibao hicho;
The video could not be loaded.