Mbunge wa Nyali na aliyekuwa ripota wa Jicho Pevu Mohammed Ali kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram amemuomboleza baba yake miaka 14 baada ya kifo chake.
Kumpoteza umpendaye ni jambo ngumu ambalo watu wengi hawalitamani kukumbana nalo.
Kupitia kwenye ujumbe wake Mohammed amekiri kwamba anampeza baba yake sana.
Huu hapa ujumbe wake Mohammed baada ya kupakia picha akiwa kwenye kaburi la baba yake.
"Siku yangu na baba yangu, baada ya maombi ya Eid, ni miaka 14 tangu atuache, miaka 14 nikitembelea kaburi lake na kumuombea
Wakati wa kutafakari na kukumbuka, nakupea sana baba," Aliandika Mohammed.