Msanii Chipukizi wa Tanzania Louis atoa EP inayofahamika kama 'Lights on me'
- Msanii chipukizi wa nyimbo za RnB kutoka Tanzania LouiS ametoa EP iliokuwa imesubiriwa sana na mashabiki wake
Msanii chipukizi wa nyimbo za RnB kutoka Tanzania LouiS ametoa EP iliokuwa imesubiriwa sana na mashabiki wake.
EP hiyo inafahamika kama 'Lights on me' kupitia EP yake msanii huyo atajitambua kama anaweza katika tasnia ya burudani au la.
EP yake ina nyimbo 6.KOna, Hennessy, Unanimaliza,leo,sawa na lost ni EP ambayo imezalishwa na wazalishaji maarufu Tanzania S2kizzy na Trone.
Huku akizungumzia EP yake alikuwa na haya ya kusema;
"Najivunia sana na nina shukrani kuu kufanya kazi na wazalishaji wa kushangaza katika EP yangu nimekuwa shabiki wao mkubwa licha yao kupewa majukumu ya nyimbo ambazo zitafahamika na zitavuma sana Afrika Mashariki
Pia kuwa na lebo na timu yangu katika kufanya kazi yangum kama wewe ni shabiki wa nyimbo basi uko katika mahali pema, furahini," Alisema Louis.
Louis alikuzwa mjini Dar Es salaam Tanzania ambapo alipenda muziki huku akijiunga na kwaya katika shule ya upili.
Akiwa katika shule ya upili Louis alipenda nyimbo za wasanii kama Wizkid,Chris Brown miongoni mwa wengine na hata kutamani miundo, na maudhui ya nyimbo zao.
Msanii huyo alianza kuimba kama njia ya kujifurahisha lakini akajipata anapenda muziki.
Akiwa kwenye chuo kikuu, Louis alisam kwamba ni wakati ambao ulikuwa mggumu kwani alikuwa anasoma na pia kujaribu kuimba.
Ana shahada ya kwanza katika akaunti
Huu hapa wimbo wake unafahamika kama KOna;
The video could not be loaded.