AIBU YA EMBARAMBAMBA
Embarambamba taabani baada ya kurekodiwa akishiriki densi chafu na mashabiki
Video inayoonyesha Embarambamba kwenye klabu akiwa amelaza mwanadada chini na kuchezea densi juu yake inazunguka mitandaoni
• Mkurugenzi mtendaji wa bodi ya uainishaji wa Filamu nchini Kenya (KFCB Ezekiel Mutua amesema tendo hilo ni la aibu na kuwa Embarambamba amevuka mipaka
•Video zinazoonyesha Embarambamba kwenye klabu akishiriki densi zisizo na maadili zinazunguka mitandaoni
Mwanamuziki wa nyimbo za injili Christopher Nyangwara almaarufu kama Embarambamba amekashifiwa sana baada ya video zinazomuonyesha mwanamuziki huyo akicheza densi za aibu kusambazwa mtandaoni.
Kwenye video hizo, Embarambamba alionekana kujiachilia kwenye klabu na kucheza na wanadada kwa mitindo isiyo ya Kikristo.
"Embarambamba.. hiyo ni aibu. Umepita mipaka sasa!" Mutua aliandika.
Mtangazaji wa habari za NTV, Lofty Matambo pia ameeleza masikitiko yake baada ya kuziona video zile.
"Nimesikitishwa sana na Embarambamba kama mmoja wa waliomshika mkono na hata kumhoji kwenye televisheni ya kitaifa. Video inayozunguka haikaribiani kabisa na anachojifanya kuwa, ati mwanamuziki wa nyimbo za injili" Matambo aliandika.