AIBU YA EMBARAMBAMBA

Embarambamba taabani baada ya kurekodiwa akishiriki densi chafu na mashabiki

Video inayoonyesha Embarambamba kwenye klabu akiwa amelaza mwanadada chini na kuchezea densi juu yake inazunguka mitandaoni

Muhtasari

• Mkurugenzi mtendaji wa bodi ya uainishaji wa Filamu nchini Kenya (KFCB Ezekiel Mutua amesema tendo hilo ni la aibu na kuwa Embarambamba amevuka mipaka

•Video zinazoonyesha Embarambamba kwenye klabu akishiriki densi zisizo na maadili zinazunguka mitandaoni

Embarambamba
Embarambamba
Image: Hisani

Mwanamuziki wa nyimbo za injili Christopher Nyangwara almaarufu kama Embarambamba amekashifiwa sana baada ya video zinazomuonyesha mwanamuziki huyo akicheza densi za aibu kusambazwa mtandaoni.

Kwenye video hizo, Embarambamba alionekana kujiachilia kwenye klabu na kucheza na wanadada kwa mitindo isiyo ya Kikristo.

Video moja haswa iliyomuonyesha msanii huyo akiwa amemlaza mwanadada chini na kuchezea juu yake ilikashifiwa sana huku wanamitandao wengi wakisema kuwa mwanamuziki huyo kweli amepotea njia sasa.

Kati ya walioonyesha kutoridhishwa kwao na video hizo ni pamoja na Mkurugenzi mtendaji wa bodi ya uainishaji wa Filamu nchini Kenya(KFCB), Ezekiel Mutua ambaye alisema kuwa kitendo hicho ni cha aibu sana.

"Embarambamba.. hiyo ni aibu. Umepita mipaka sasa!" Mutua aliandika.

 

Mtangazaji wa habari za NTV, Lofty Matambo pia ameeleza masikitiko yake baada ya kuziona video zile.

"Nimesikitishwa sana na Embarambamba kama mmoja wa waliomshika mkono na hata kumhoji kwenye televisheni ya kitaifa. Video inayozunguka haikaribiani kabisa na anachojifanya kuwa, ati mwanamuziki wa nyimbo za injili" Matambo aliandika.

Video ingine inayomuonyesha Embarambamba ameinua shabiki mmoja juu na kumuekelea kwa kiuno chake kisha kucheza densi naye pia imeibua gumzo sana mtandaoni.

Baadhi ya Wakenya walisema kuwa huo ndio ulikuwa mwanzo wa kuanguka kwa mwanamuziki huyo aliyepata umaarufu mkubwa kutoka na sarakasi anazofanya kwenye nyimbo zake.