Je, sarakasi za Embarambamba zinahatarisha maisha yake?

Embarambamba amewachilia video mpya inayomshirikisha kukimbia kwenye barabara iliyo na magari

Muhtasari

Embarambamba amewachilia video mpya inayomshirikisha kukimbia kwenye barabara iliyo na magari

Embarambamba akiwa kwenye sarakasi zake
Embarambamba akiwa kwenye sarakasi zake
Image: HISANI; YOUTUBE

Wimbo mpya wa msanii wa nyimbo za injili, Christopher Nyangwara, almaarufu kama Embarambamba ‘nimeanza safari’ umepokelewa na hisia mbalimbali.

Video ya mwanamuziki huyo akinusurika kugongwa na bodaboda iliyokuwa ikisambazwa mtandaon kabla ya kutolewa kwa wimbo iliibua gumzo sana mtandaoni huku Wakenya wakimwagiza Embarambamba kuwa makini anapocheza sarakasi zake.

Kwenye wimbo huo uliowekwa kwenye mtandao wa Youtube siku ya jumanne, mwanamuziki huyo mwenye mitindo ya densi ya  kustaajabisha  ameonekana kukimbia kwenye barabara iliyo na magari kutoka upande mmoja hado mwingine huku magari yakipita.

Mwanamuziki huyo tokea Nyamira amepata umaarufu mkubwa mno kutokana na sarakasi zinazoambatana na densi zake. Wengi wamestaajabishwa na sarakasi zile huku wengine wakikisia kwamba huenda anahitaji huduma za mtaalamu wa kisaikolojia.

Embarambamba ameendelea kupata umaarufu mkubwa huku akipata mikataba na baadhi ya kampuni tajika.