In Summary

•“Nilichoka na unafiki uliokuwa kwenye sekta ya injili. Tena nilitaka kuwa mkweli na kutodanganya Mungu. Mungu hawezi danganywa kwa hivyo nilitulia na sasa niko hapa. Wale watu ambao hawakunitaka kwenye sekta ya injili ndio walikuwa wa kwanza kunifikia nilipohama” Alikiri Willy Paul.

Willy Paul
Image: Instagram

Mwanamuziki Wilson Radido almaarufu kama Willy Paul amesema kuwa chuki, ubaguzi, mapendeleo na ngoma zake kukosa kuchezwa ndio sababu aligura sekta ya injili.

Kupitia mtandao wa Instagram, msanii huyo ambaye alianza kama mtunzi wa nyimbo za injili kabla ya kugeukia nyimbo za kidunia miaka miwili iliyopita amesema kuwa kufikia kuhuma huko alikuwa amezama katika hali ya huzuni, jambo ambalo lilimfanya kugeuka fukara asiyeweza kutumikia mahitaji yake ya kinyumbani.

Sababu kwanini niliondoka, chuki kutoka kwa wasanii wenzangu na wacheza santuri, nyimbo zangu kukosa kuchezwa kwa madai kuwa hazikuwa za Mungu, ubaguzi, mapendeleo.. nilikuwa msanii bora ila watu hao waovu hawangeona hivyo ama waliamua tu kupuuza ukweli. Walivunja moyo wangu! Waliniumiza vibaya! Nilipatwa na huzuni kwa kipindi cha miezi nne. Nililia pekee yangu kila mchana na usiku. Ilifikia wakati singevumilia tena.. sikuwa na pesa za kulipa bili zangu na kukimu mahitaji yangu pale nyumbani” Willy Paul aliandika.

Ameeleza kuwa alipitia wakati mgumu sana alipokuwa anaimba nyimbo za injili

Mimi si kamili ila niliyoyapitia kama msanii wa injili, hakuna  mtumishi yeyote wa Mungu anafaa kupitia" Alisema Paul

Mwanamuziki huyo amesema kuwa ndoto na mapenzi yake kwa muziki zilimfanya kuvuka kutoka injili na kuanza kutengeneza nyimbo za kidunia.

“Nilichoka na unafiki uliokuwa kwenye sekta ya injili. Tena nilitaka kuwa mkweli na kutodanganya Mungu. Mungu hawezi danganywa kwa hivyo nilitulia na sasa niko hapa. Wale watu ambao hawakunitaka kwenye sekta ya injili ndio walikuwa wa kwanza kunifikia nilipohama” Alikiri Willy Paul.

Willy Paul alisema kuwa ameshuhudia mengi ikiwemo kusalitiwa na marafiki na familia ila bado anasimama. Amewasuta wanaomchukia bila sababu.

View Comments