Kupitia ujumbe alioandika kwenye mtandao wa Instagram, Bahati amehakikishia Mungu kuwa bado ameshikilia ahadi kuwa hatawahi muacha ambayo alimpatia alipokuwa anapokea tuzo la Groove.
"Naapa mbele ya dunia, Mungu sitawahi kuacha" Bahati alisema kwa wakati ule.
Nyimbo za Bahati za hivi karibuni zimeibua gumzo kubwa haswa mitandaoni huku wengi wakidai kuwa mwanamuziki huyo amegura injili.
Hata hivyo, Bahati amejitetea na kusema kuwa yeye ni yule yule na hajabadilika.
"Nimeona watu wengi wakinitumia na kunitaja kwenye video hii (iliyoambatana na ujumbe wake). Lakini Mungu wajua roho yangu na wajua kuwa huyu bado ni mimi. Haya bado ni maneno yangu na wajua sijawahibadilika. Endelea kunishika mkono ninapopeleka muziki wa Kenya kote duniani" Bahati aliandika.
Kwa sasa mwanamuziki huyo yumo nchini Tanzania kurekodi video ya wimbo mmoja kwenye albamu yake ambao alishirisha mwanamuziki tajika wa bongo, Rayvanny. Bahati aliandamana na mpenzi wake, Diana Marua.