In Summary

•Mwanamuziki Willy Paul ametoa wimbo wa kumtusi nyota wa Bongo Diamond.

•'Kamata, jicho kwa jicho, jino kwa jino" Paul alikuwa ameapa kwenye mtandao wa Instagram.

Willy Paul
Image: Hisani

Mwanamuziki Willy Paul ametoa wimbo wa kumtusi nyota wa Bongo Diamond.

Willy Paul amekuwa akimkashifu Diamond kwa madai kuwa aliiba mawazo ya wimbo wake 'Nikune' ambao alishirikisha Nadia Mukami  katika utunzi wa  wimbo 'Kamata' ambao alitoa juzi.

Mwanamuziki huyo ambaye aligura sekta ya injili takriban miaka miwili iliyopita alikuwa ameahidi kuwa  atatoa wimbo unaofanana na ule wa Diamond ili kulipiza kisasi.

'Kamata, jicho kwa jicho, jino kwa jino" Paul alikuwa ameapa kwenye mtandao wa Instagram.

"Simba, hakuna yeyote ambaye anamuibia mfalme. Nitakata kichwa chako" Willy Paul aliandika kwenye chapisho lingine kabla ya kutoa wimbo wake.

Hatimaye asubuhi ya Jumatano ametekeleza ahadi yake na kupakia wimbo uliojaa matusi yanayoelekezewa Diamond.

The video could not be loaded.

#willypaul #kamata #saldidointernational
Willy Paul alimwandikia Diamond kuwa wasizoeane na asitishe mambo ya kuibiana mawazo na kudharau wengine.

"Tusizoeane , kama mbaya mbaya! Mambo ya kuibiana mawazo na kuwa na dharau lazima iishe" Paul alisema.

Diamond aliachilia kibao kipya 'Kamata' siku tano zilizopita na ndicho kimeibua mzozo na Willy Paul.

The video could not be loaded.

Click Below To Get #Kamata Song Now! 👇🏻 https://dplatnumz.lnk.to/kamata Diamond Platnumz has released his new single dubbed ‘’Kamata’’, a combination of Afropop and Bongo Fleva. It's a dance song and a banger and is expected to make waves in clubs across Africa! Diamond Platnumz Booking Info: Email:bookplatnumz@gmail.com | sallam.sharaff@gmail.com Catch Up With Diamond Platnumz On: Instagram:https://www.instagram.com/diamondplatnumz/ Facebook:https://www.facebook.com/DiamondPlatnumz255/ Twitter:https://twitter.com/diamondplatnumz/ #Diamondplatnumz #Wasafi #Kamata
Je, ni kweli aliiba mawazo ya Willy Paul?
View Comments