NANI MFALME?
Diamond na Alikiba wanazozana? Jumbe zinazoashiria kuwa huenda kuna ugomvi unaoendelea kati yao
,Jumbe za wawili hao za hivi karibuni kwenye mitandao ya kijamii zimeashiria kuwa huenda kuna ugomvi unaoendelea kati yao
•Huenda mafahari wawili wakubwa wa Bongo Diamond Platnumz na Alikiba wanazozana siku chache tu baada ya wawili hao kuachilia vibao vilivyopokelewa kwa kishindo na mashabiki wao
•Kwa miaka mingi wawili hao ambao wana ufuasi mkubwa kweli nchini Tanzania na kote Afrika wamedhaniwa kuwa na ugomvi kuhusu nani nyota kuliko mwingine ila hawajadhihirisha hayo hadharani.
Huenda mafahari wawili wakubwa wa Bongo Diamond Platnumz na Alikiba wanazozana siku chache tu baada ya wawili hao kuachilia vibao vilivyopokelewa kwa kishindo na mashabiki wao.
Diamond aliachilia kibao kwa jina IYO siku ya Alhamisi alafu siku moja baadae Alikiba akawachilia kibao chake Jealous alichoshirikisha mwanamuziki Mayorkun kutoka Nigeria.
The video could not be loaded.
Nyimbo hizo zote mbili ziliweza kupata watazamaji zaidi ya milioni moja kwa siku moja. Hata hivyo kibao cha Alikiba ambacho kiliwachiliwa baada ya cha Diamond kimepata watazamaji wengi kushinda kile cha Diamond kufikia sasa.
Kufikia sasa wimbo 'IYO' wake Diamond umetazamwa na watu milioni 2.9 ilhali 'Jealous' chake Alikiba kimetazamwa na watu milioni 3.2.
Licha ya kuwa kibao cha Alikiba kinaongoza kwa nambari ya watazamaji, kile cha Diamond kinaongoza kwenye orodha ya ngoma zinazovuma sana nchini kwa sana kwenye mtandao wa Youtube huku cha Alikiba kikiorodheshwa katika nambari ya kumi.
The video could not be loaded.
Kwa miaka mingi wawili hao ambao wana ufuasi mkubwa kweli nchini Tanzania na kote Afrika wamedhaniwa kuwa na ugomvi kuhusu nani nyota kuliko mwingine ila hawajadhihirisha hayo hadharani.
Hata hivyo, jumbe za wawili hao za hivi karibuni kwenye mitandao ya kijamii zimeashiria kuwa huenda kuna ugomvi unaoendelea kati yao.
Mnamo Jumapili mida ya alasiri Diamond alipakia video ya mashabiki wakifurahia wimbo wake na kuambatanisha na ujumbe wenye maana fiche ulioonekana kuelekezwa kwa Kiba.
"Kielelezo halisi ya kibao kikubwa na wimbo pendwa.. ubaya wa vyakununua haupati vitu kama hivi.." Diamond aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram.
Takriban masaa mawili baadae Alikiba alipakia video ya mwanamuziki Stevo Simple Boy akisema "Inauma but inabidi uzoee.."
Hata kama aliambatanisha video hiyo na ujumbe kuwa collabo na Simple Boy yaja, baadhi ya mashabiki wa muziki wa Bongo wamekadiria kuwa ujumbe huo ni jibu la Kiba kwa Diamond.
Ingawa wawili hao hawajakiri kuhusu ugomvi wao, ni dhahiri kuwa kunazo tofauti kadhaa kati yao.
Hata hivyo, Ali Kiba alipokuwa nchini Kenya hivi majuzi akiwa kwenye mahojiano na Jalango katika kipindi cha Bonga na Jalas alidai kuwa hapendi kuwa na ugomvi na yeyote.
Alisema kuwa yeye hashindani na yeyote na kazi anayofanya ni tofauti.