NANI MFALME?

Diamond na Alikiba wanazozana? Jumbe zinazoashiria kuwa huenda kuna ugomvi unaoendelea kati yao

,Jumbe za wawili hao za hivi karibuni kwenye mitandao ya kijamii zimeashiria kuwa huenda kuna ugomvi unaoendelea kati yao

Muhtasari

•Huenda mafahari wawili wakubwa wa Bongo Diamond Platnumz na Alikiba wanazozana siku chache tu baada ya wawili hao kuachilia vibao vilivyopokelewa kwa kishindo na mashabiki wao

•Kwa miaka mingi wawili hao ambao wana ufuasi mkubwa kweli nchini Tanzania na kote Afrika wamedhaniwa kuwa na ugomvi kuhusu nani nyota kuliko mwingine ila hawajadhihirisha hayo hadharani.

Image: INSTAGRAM

Huenda mafahari wawili wakubwa wa Bongo Diamond Platnumz na Alikiba wanazozana siku chache tu baada ya wawili hao kuachilia vibao vilivyopokelewa kwa kishindo na mashabiki wao.

Diamond aliachilia kibao kwa jina IYO siku ya Alhamisi alafu siku moja baadae Alikiba akawachilia kibao chake Jealous alichoshirikisha mwanamuziki Mayorkun kutoka Nigeria.

Stream & Download IYO On 👇🏻 https://dplatnumz.lnk.to/iyo Let's Get Our Dance Moves Together And Party Till The Sun Rises Diamond Platnumz Booking Info: Email:bookplatnumz@gmail.com | sallam.sharaff@gmail.com Catch Up With Diamond Platnumz On: Instagram:https://www.instagram.com/diamondplatnumz/ Facebook:https://www.facebook.com/DiamondPlatnumz255/ Twitter:https://twitter.com/diamondplatnumz/ #Diamondplatnumz #Amapiano #Iyochallenge

Nyimbo hizo zote mbili ziliweza kupata watazamaji zaidi ya milioni moja kwa siku moja. Hata hivyo  kibao cha Alikiba ambacho kiliwachiliwa baada ya cha Diamond kimepata watazamaji wengi kushinda kile cha Diamond kufikia sasa.

Kufikia sasa wimbo 'IYO' wake Diamond umetazamwa  na watu milioni 2.9 ilhali 'Jealous' chake Alikiba kimetazamwa na watu milioni 3.2.

Licha ya kuwa kibao cha Alikiba kinaongoza kwa nambari ya watazamaji, kile cha Diamond kinaongoza kwenye orodha ya ngoma zinazovuma sana nchini kwa sana kwenye mtandao wa Youtube huku cha Alikiba kikiorodheshwa katika nambari ya kumi.

Music Video by Alikiba featuring Mayorkun performing Jealous {Album Single}. (C) 2021 exclusively licensed Under (Alikiba) from Ziiki Media (PTY) & Kings Music Records, The Music Video was shot in Lagos - Nigeria, Directed by Pink. Stream/Download: https://smartklix.com/Jealous(feat.Mayorkun)02 Click here URL:https://ffm.to/alikibajealous Listen to Alikiba on: Audiomack: https://audiomack.com/alikiba Apple Music: https://music.apple.com/us/artist/alikiba/578354001 Boomplay: https://www.boomplay.com/share/artist/2051126 YouTube: https://www.youtube.com/c/AlikibaOfficial Spotify: https://open.spotify.com/artist/2nGoKcLdXktxEXvMdTDsIT Connect with Alikiba on Social Media: Instagram:https://Instagram.com/officialalikiba​ Facebook:https://web.facebook.com/OfficialAlikiba​ Twitter:https://twitter.com/officialAlikiba/​ TikTok:https://vm.tiktok.com/ZSmuTQ2W/​ Connect with Mayorkun on Social Media: Instagram:https://instagram.com/iammayorkun Facebook:https://web.facebook.com/mayorkunofficial Twitter:https://twitter.com/iammayorkun Website:http://mayorkun.com The Official YouTube Channel Of Alikiba. Subscribe for the Latest Music Videos, Performances, and More.https://www.youtube.com/c/AlikibaOfficial +For More Information Booking Alikiba: Contact:emailalikiba@gmail.com Manager:Aidancharlie1@gmail.com #Alikiba #Mayorkun #Jealous ©2021 Ziiki Media & Kings Music Records.All rights reserved.

Kwa miaka mingi wawili hao ambao wana ufuasi mkubwa kweli nchini Tanzania na kote Afrika wamedhaniwa kuwa na ugomvi kuhusu nani nyota kuliko mwingine ila hawajadhihirisha hayo hadharani.

Hata hivyo, jumbe za wawili hao za hivi karibuni kwenye mitandao ya kijamii zimeashiria kuwa huenda kuna ugomvi unaoendelea kati yao.

Mnamo Jumapili  mida ya alasiri Diamond alipakia video ya mashabiki wakifurahia wimbo wake na kuambatanisha na ujumbe wenye maana fiche  ulioonekana kuelekezwa kwa Kiba.

"Kielelezo halisi ya kibao kikubwa na wimbo pendwa.. ubaya wa vyakununua haupati vitu kama hivi.." Diamond aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Takriban masaa mawili baadae Alikiba alipakia video ya mwanamuziki Stevo Simple Boy akisema "Inauma but inabidi uzoee.."

Hata kama aliambatanisha video hiyo na ujumbe kuwa collabo na Simple Boy yaja, baadhi ya mashabiki wa muziki wa Bongo wamekadiria kuwa ujumbe huo ni jibu la Kiba kwa Diamond.

Ingawa wawili hao hawajakiri kuhusu ugomvi wao, ni dhahiri kuwa kunazo tofauti kadhaa kati yao.

Hata hivyo, Ali Kiba alipokuwa nchini Kenya hivi majuzi akiwa kwenye mahojiano na Jalango katika kipindi cha Bonga na Jalas alidai kuwa hapendi kuwa na ugomvi na yeyote.

Alisema kuwa yeye hashindani na yeyote na kazi anayofanya ni tofauti.