Ex wa Jose Chameleone ameanzisha chaneli YouTube kwa jina 'Diary of a Retired Wie'

Alisema atashiriki uzoefu wa miaka 16 ya ndoa na mwimbaji Jose Chameleone ambaye wana watoto watano. Anaamini kilichompata kinatokea kwa wanawake wengi ambao hawana sauti. "Hatuachi chochote nje," alisema.

Muhtasari

• Hata hivyo, kilichowashangaza wengi ni hatua ya kuita kipindi chake kwenye chaneli hiyo kuwa ‘Diary of a retired wife’ kwa maana kwamba atakuwa anazungumzia ratiba ya mke aliyestaafu kutoka kwa ndoa.

• Katika video akiitambulisha chaneli, Daniella Atim alisema atashiriki uzoefu wake ili wanawake wajifunze kutoka kwao na kuwezeshwa.

Atim na Chameleone
Atim na Chameleone
Image: Hisani

Aliyekuwa mke wa msanii kutoka Uganda Jose Chameleone, Daniella Atim amejitosa mazima katika ukuzaji maudhui kwenye mtandao wa YouTube.

Atim amezindua chaneli yake ya YouTube ambayo ameweka wazi kwamba atakuwa anazungumzia maudhui yanayohusiana na ndoa, mambo mazuri na mabaya yaliyotokea wakati wa uchumba na kuolewa na Jose Chameleone hadi kufikia hatua ya kutengana.

Atim na hitmaker huyo wa ‘Badilisha’ walikuwa wameoana kwa miaka 16.

Hata hivyo, kilichowashangaza wengi ni hatua ya kuita kipindi chake kwenye chaneli hiyo kuwa ‘Diary of a retired wife’ kwa maana kwamba atakuwa anazungumzia ratiba ya mke aliyestaafu kutoka kwa ndoa.

Katika video akiitambulisha chaneli, Daniella Atim alisema atashiriki uzoefu wake ili wanawake wajifunze kutoka kwao na kuwezeshwa.

Alisema programu za kitamaduni za sasa zinawazuia wanawake kuzungumza dhidi ya wanaume, hata wale wanaohusiana nao. Alisema anataka kutoa jukwaa la kukabiliana na masuala ambayo yanachukuliwa kuwa mwiko.

Alisema atashiriki uzoefu wa miaka 16 ya ndoa na mwimbaji Jose Chameleone ambaye wana watoto watano. Anaamini kilichompata kinatokea kwa wanawake wengi ambao hawana sauti. "Hatuachi chochote nje," alisema.

Alisema atazungumza kila kitu, kuanzia jinsi alivyokutana na mumewe hadi mwisho.

Kupitia Instagram mwezi Machi, Daniella Atim alisema amekuwa Marekani kwa miaka mitano, akitaja unyanyasaji wa nyumbani kama sababu kuu ya kuvunjika kwa ndoa yake na msanii huyo.

Katika chapisho lililotajwa hapo juu, aliangalia nyuma matukio ya kuhuzunisha ya ndoa yake ambayo hatimaye yalimfukuza kutoka kwa baba wa watoto wake.

Katika Instagram story, Atim alifichua jinsi alivyovumilia mateso ya miaka 16 ya unyanyasaji wa nyumbani.

Sasa anaishi Minnesota pamoja na watoto wake wote, Atim alizungumzia matatizo yake kama mama asiye na mwenzi na jitihada yake ya kupata maisha salama, yenye furaha na yenye kuridhisha zaidi.