(Video) Sina Neno! Jux amwandikia wimbo aliyekuwa mpenzi wake Vanessa Mdee kumpongeza kwa ujauzito, asema hana chuki
•Jux amesema kuwa ana raha sana kuona kwamba Mdee anafurahia ndoa yake ya sasa na mwigizaji Rotimi na kumpongeza kwa kuwa hivi karibuni ataweza kuitwa mama.
•Msanii huyo amesema kuwa hana chuki yoyote na Mdee na kudai kuwa anamwombea maisha ya furaha pamoja na mpenzi wake. Amewashauri wavumiliane na wasiwahi kugombana ili mtoto wao asiwahi pata shida.
Staa wa Bongo Juma Jux ametoa wimbo wa kumpongeza aliyekuwa mpenzi wake Vanessa Mdee baada yake kutangaza kuwa ni mjamzito
Kwenye wimbo 'Sina Neno' ambao alipakia kwenye mtandao wa Youtube siku ya Jumatano, Jux amemhakikishia Mdee kuwa hana ugomvi wowote na yeye kwani alishafunika yaliyopita kwenye kaburi la sahau.
Jux amesema kuwa ana raha sana kuona kwamba Mdee anafurahia ndoa yake ya sasa na mwigizaji Rotimi na kumpongeza kwa kuwa hivi karibuni ataweza kuitwa mama.
"Naona wameremeta, ngozi imenawili una furaha now,
Kitanda hakina siri, zao la tendo una kitumbo wow,
Mnapendeza sana na penzi liko kasi kasi
Mkipostiana, Instagram status..." Jux amesema kwenye wimbo huo.
Msanii huyo amesema kuwa hana chuki yoyote na Mdee na kudai kuwa anamwombea maisha ya furaha pamoja na mpenzi wake. Amewashauri wavumiliane na wasiwahi kugombana ili mtoto wao asiwahi pata shida.
"Najua una furaha kwa zawadi uliyopata.
Tena ulivyo shujaa,mtoto mama amepata.
Na nyie msije gombana, mtoto asije akapata kash kash
Uzuri kuvumiliana, matatizo mkadiscuss
Tulishafunika kurasa, mambo ya zamani yalishapita
Maisha mengine sasa, kuwa na amani hakuna vita
Sikuchukii nakuombea,
Maisha mema ya furaha, Mungu awaonyeshe njia
Siumii, nimezoea, ila nina furaha kuiona familia
Niko salama, Mimi sina neno" Jux amesema
The video could not be loaded.