Rick Ross aweka wazi uhusiano wake na Hamisa Mobetto
- Rick Ross aweka wazi uhusiano wake na Hamisa Mobetto
Mwimbaji wa hip hop wa Marekani Rick Ross hatimaye ameibuka na kuzungumzia uhusiano wake na Hamisa Mobetto.
Alithibitisha kuwa walikuwamarafiki wa karibu sana, wala hakufafanua ukaribu wa uhusiano wao huku akisema kwamba atamwachia Hamisa afafanue uhusiano wao.
Uvumi wa urafiki wao ulienea sana baada ya rappa huyo, kutoa maoni kenye picha za Hamisa alizokuwa anapakia kwenye ukurasa wake wa instagram, huku mashabiki wakisema kwamba wawili hao ni wapenzi.
Wawili hao pia walionekana karibu mwezi au miwili iliyopita huko Dubai na wanamitandao kudai wanaweza kuwa kwenye likizo.
Katika mahojiano na Lil Ommy, Rapa na mfanyabiashara aliyeshinda Tuzo aliongeza kuwa yuko tayari kumuunga mkono Mobetto kutimiza ndoto zake zote kwa sababu yeye ni mjasiriamali mzuri.
"Lazima niseme ukweli, kuna uhusiano, ni kiasi gani unataka nitakuambia juu yake?, Nitamwachia yeye… lakini yeye ni mtu mzuri sana, mrembo roho na yeye ni mjasiriamali mkubwa na ninataka kumsaidia kuipeleka katika kiwango kingine kwa sababu anafanya kazi nzuri na ninajivunia.
Kuna mambo mengine kadhaa lakini yote kwa yote nataka kumuona akishinda ”alisema Rick Ross.
The video could not be loaded.
Rick Ross pia alisema kuwa ana mpango wa kutembelea Tanzania hivi karibuni.