In Summary

•Mwanadada huyo mwenye umri wa miaka 31 amesema kwamba kunao watu ambao wamewahi kujaribu kumuua ila kwa neema zake Mungu hawajaweza kufaulu.

•Amedai kwamba kuna baadhi ya watu ambao hawakuridhishwa na ujauzito wake na tangu alipoufichua  wamekuwa wakiomba kila uchao msiba umpate.

•Vera ameendelea kudai kwamba watu wale wenye roho mbaya kwa sasa wanadai atapoteza maisha yake wakati atakuwa anajifungua kuona kuwa maombi yao mabaya hayajaweza kufaulu kufikia sasa.

Image: INSTAGRAM

Mwanasoshaliti mashuhuri Vera Sidika amesema kwamba kwa miaka mingi sasa kuna watu wengi  wenye nia mbaya na maisha yake ambao wamekuwa wakimuandama.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, mwanadada huyo mwenye umri wa miaka 31 amesema kwamba kunao watu ambao wamewahi kujaribu kumuua ila kwa neema zake Mungu hawajaweza kufaulu.

"Kama ni kifo, kwa miaka mingi watu wamejaribu. Lakini bado niko hapa kwa neema zake Mungu. Sio wakati wako hadi Mungu atakapoamua ni wakati wako. Binadamu watasema, wajaribu kufanya kila kitu ili wakuangamize lakini kama sio wakati wako hakuna chochote wafanyacho kinajalisha. Mungu ako nami hata mkinitumia maovu ya aina yote kila siku bado nayaepuka" Vera alisema.

Amedai kwamba kuna baadhi ya watu ambao hawakuridhishwa na ujauzito wake na tangu alipoufichua  wamekuwa wakiomba kila uchao msiba umpate.

Mama huyo mtarajiwa amedai kuna watu ambao walisema ujauzito wake ungeharibika punde baada yake kuufichua lakini nguvu za Mola zikamsaidia kuepuka laana zao.

"Wengine hata walisema ujauzito wangu ungeharibika punde baada ya kuufichua. Eti nitapoteza mtoto wangu kama bado hajazaliwa. Mambo mengi. Kama wangekuwa na nguvu nyingi kuliko Mungu , mbona wasiyatekeleze. Sasa tuko na ujauzito wa miezi nane unusu kwa sababu ya Mungu. Kila siku anaendelea kuwatia aibu" Alisema Vera.

Vera ameendelea kudai kwamba watu wale wenye roho mbaya kwa sasa wanadai atapoteza maisha yake wakati atakuwa anajifungua kuona kuwa maombi yao mabaya hayajaweza kufaulu kufikia sasa.

Hata hivyo amedai kuwa bado ako imara kwani anaamini nguvu za Maulana zinamlinda.

"Sasa  wamehitimu wanadai eti nitafariki wakati nitakuwa najifungua mtoto wangu. Yale maovu ambayo watu wananitakia na kuniambia usoni!! Hebu tafakari mtu akichukua muda wake kuandikia mwanamke mjamzito ujumbe kama huo" Alisema.

Mwanasoshalaiti huyo amesema kwamba ujasiri wake ndio umemsaidia kubaki imara licha ya maovu ambayo watu wamekuwa wakimtakia na kumwambia.

View Comments