In Summary
  • Aliyekuwa Meneja wa Tanasha  Donna afichua aliyoyapitia Tanasha baada ya kuachana na Diamond

African Castro, aliyekuwa meneja wa Tanasha Donna alisema kuwa mama huyo wa mtoto mmoja alipaswa kutafuta usaidizi wa kitaalamu baada ya kuachana na Diamond.

Akizungumza wakati wa mahojiano na Presenter Ali, Castro alisema kutengana huko kulifanya Tanasha kukosa mwelekeo.

"Drama ya  uhusiano uliathiri kasi tuliyokuwa nayo. Ukweli ni kwamba Tanasha aliumia baada ya kuachana na Diamond na hakupumzika kutafuta msaada kutoka kwa mtaalamu

Hapo ndipo niliponawa mikono yangu na kumuacha kwa meneja wake mwingine. Nilikutana na Tanasha alipokuwa mwanamitindo," Alio ngea Castro.

Aliongeza kuwa Tanasha amepitia mengi, na kuwa hawezi andika kitabu bila kumtaja Castro.

"Alifanya Tangazo na Safaricom na ndipo alipojulikana, baada ya hapo akaenda NRG,Kuna mengi ninaweza kusema juu yake na kuna mengi anaweza kusema kunihusu lakini tuliamua kutoyazungumza

Amepitia mengi. Unachokiona sasa ni athari yangu. Hawezi kuandika kitabu bila kunitaja."

The video could not be loaded.

#presenterali #tanasha #tanashadonna
 
View Comments