In Summary

•Milly amesema katika  kipindi ambacho wamekuwa kwa ndoa amejifunza kwamba kila ndoa huwa na majaribio yake. 

•Kabi alisema mwaka huu umekuwa na majaribio mengi ambayo  yamefanya wakakua kama wanandoa.

Image: INSTAGRAM// KABI WAJESUS

Leo hii , (Desemba 2, 2021) wanavlogu maarufu Peter Kabi na Millicent Wambui  wa 'The Wajesus Family'  wanaadhimisha miaka minne katika ndoa.

Wanandoa hao ambao hujitambulisha kama Kabi na Milly Wajesus wamechugua kisiwa cha Mauritius kama eneo bora la kufanya maadhimisho yao ya ndoa.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Kabi alieleza kwamba waliamua kufanya maadhimisho yao nchini Mauritius kwani ni ndoto ya mkewe kuenda likizo pale.

"Niliamua kupeleka mpenzi wangu kwa eneo la likizo la ndoto lake tunapoadhimisha miaka minne katika ndoa" Kabi alisema.

Kabi alisema Mungu amekuwa mwaminifu sana kwao katika kipindi ambacho wamekuwa pamoja huku akitarajia kuendelea kutengeneza kumbukumbu zaidi na mpenzi wake.

Milly kwa upande wake amesema katika  kipindi ambacho wamekuwa kwa ndoa amejifunza kwamba kila ndoa huwa na majaribio yake. Aliwasihi wanandoa wasikubali shetani aporomoshe ndoa  zao kufuatia majaribio watakayopitia. 

"Kile ambacho nimejifunza miaka hiyo ni kuwa kila kiapo cha ndoa kitajaribiwa.  Usikubali shetani ashinde. Huwezi jaribiwa kwa namna ambayo hutawezana" Alisema Milly.

Walipokuwa kwenye mahojiano na SPM Buzz kabla ya kuenda Mauritius, Kabi alisema mwaka huu umekuwa na majaribio mengi kwao na yamefanya wakakua kama wanandoa.

Alisema miaka ya hapo awali ilikuwa nyororo sana kwao lakini mwaka huu wamepitia mengi ila bado wako imara.

"Kusema kweli  hatuwezi linganisha mwaka huu na mwaka mwingine. Huu ndio mwaka ambao tumekuwa na misukosuko mingi na mambo mengi ya kushughulikia. Mwaka huu umefanya tukakua kama wanandoa. Miaka hiyo mingine ilikuwa rahisi sana. Miaka mitatu ya hapo awali kila kitu kilikuwa kinaenda nyororo hadi mwaka huu ambao tulikuwa na changamoto mitandaoni. Lakini hatujatengana kama wanandoa na bado tuko imara" Alisema Kabi.

Wanandoa hao wawili walishambuliwa sana mapema mwaka huu wakati Kabi alikiri kuwa na binti ambaye alipata na binamu yake miaka saba iliyopita.

View Comments