'Umezeeka oa sasa,'Eric Omondi amwambia nduguye huku akisherehekea siku yake ya kuzaliwa
- Baadhi ya Wakenya walimkejeli wakisema anapaswa kuoa kwanza kama mfano kwa mdogo wake
Erick Omondi ni mmoja wa watu mashuhuri wa Kenya ambaye amekuwa akiwashangaza mashabiki wake kila siku kutokana na vipaji vyake vya kipekee pamoja na ubunifu.
Mchekeshaji huyo amejishindia mamilioni ya wafuasi katika kurasa zake rasmi za mitandao ya kijamii wanaopenda, kufuatilia na kutazama machapisho yake kila siku.
Dakika chache zilizopita Erick Omondi ametuma ujumbe wa siku ya kuzaliwa kwa mdogo wake, mcheshi Fred Omondi.
Alimtakia heri ya siku ya kuzaliwa na kufurahiya kwa wingi huku akiahidi kujumuika naye kwa tafrija leo jioni.
Hata hivyo, matamshi ya mwisho ya Erick Omondi yalionekana kupingana huku akimshauri kakake kuoa sasa, ilhali bado hajaoa ingawa yeye ndiye kaka yake mkubwa.
Baadhi ya Wakenya walimkejeli wakisema anapaswa kuoa kwanza kama mfano kwa mdogo wake.
"Happy BIRTHDAY BROπ₯π₯π₯³π₯³π₯³π₯³π₯³π€ π€ π€ Umezeeka Oa sasa pleaseπππ. Naskia leo kuna Sherehe hapo Kifaru place lazima ntapitia. @fredomondi_," Aliandika Eric.
Hizi hapa baadhi ya hisia za mashabiki;
thee_nairobi_kid: Hapa mnakaa mau mau fightersππ
alex.obure: Pesa ni sabuni ya roho πππ
drummdrew: Watoto wapotevuπππππ
9.9.9jaccuzi: ππ mnafanana diffrence inakuja kwa tabia na fashion
_abed_ke: Eti utapitiaπππyou should be there man