'Umezeeka oa sasa,'Eric Omondi amwambia nduguye huku akisherehekea siku yake ya kuzaliwa

Muhtasari
  • Baadhi ya Wakenya walimkejeli wakisema anapaswa kuoa kwanza kama mfano kwa mdogo wake
eric-omondi
eric-omondi

Erick Omondi ni mmoja wa watu mashuhuri wa Kenya ambaye amekuwa akiwashangaza mashabiki wake kila siku kutokana na vipaji vyake vya kipekee pamoja na ubunifu.

Mchekeshaji huyo amejishindia mamilioni ya wafuasi katika kurasa zake rasmi za mitandao ya kijamii wanaopenda, kufuatilia na kutazama machapisho yake kila siku.

Dakika chache zilizopita Erick Omondi ametuma ujumbe wa siku ya kuzaliwa kwa mdogo wake, mcheshi Fred Omondi.

Alimtakia heri ya siku ya kuzaliwa na kufurahiya kwa wingi huku akiahidi kujumuika naye kwa tafrija leo jioni.

Hata hivyo, matamshi ya mwisho ya Erick Omondi yalionekana kupingana huku akimshauri kakake kuoa sasa, ilhali bado hajaoa ingawa yeye ndiye kaka yake mkubwa.

Baadhi ya Wakenya walimkejeli wakisema anapaswa kuoa kwanza kama mfano kwa mdogo wake.

"Happy BIRTHDAY BRO๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ๐Ÿฅณ๐Ÿฅณ๐Ÿฅณ๐Ÿฅณ๐Ÿฅณ๐Ÿค ๐Ÿค ๐Ÿค  Umezeeka Oa sasa please๐Ÿ™๐Ÿ™๐Ÿ™. Naskia leo kuna Sherehe hapo Kifaru place lazima ntapitia. @fredomondi_," Aliandika Eric.

Hizi hapa baadhi ya hisia za mashabiki;

thee_nairobi_kid: Hapa mnakaa mau mau fighters๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚

alex.obure: Pesa ni sabuni ya roho ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚

drummdrew: Watoto wapotevu๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚

9.9.9jaccuzi: ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚ mnafanana diffrence inakuja kwa tabia na fashion

_abed_ke: Eti utapitia๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚you should be there man