In Summary
  • Inasemekana kuwa mtu Mashuhuri ni kama upanga  wenye makali kwenye pande zote mbili
  • Nyota Ndogo kupitia kwenye akaunti yake ya Instagram alifunguka jinsi amekuwa akipokea kejeli  kutoka kwa mashabiki kwa ajili ya sura yake
Image: INSTAGRAM// NYOTA NDOGO

Inasemekana kuwa mtu Mashuhuri ni kama upanga  wenye makali kwenye pande zote mbili.

Hii ni kwa sababu mara moja umaarufu unakuja katika maisha ya mtu, mashabiki watawapenda na kukuchochea kwa sifa kila mahali unapoenda na kila kitu unachofanya.

Hata hivyo upendo huu kwa njia moja au nyingine unaweza kubadilika haraka kuhusiana na kile unachofanya au kile unachosema, na unaweza kwa bahati mbaya kuishia kupokea kejeli kutoka kwao

Nyota Ndogo kupitia kwenye akaunti yake ya Instagram alifunguka jinsi amekuwa akipokea kejeli  kutoka kwa mashabiki kwa ajili ya sura yake.

Kulingana na Nyota wengi wanaomkejeli ni wanaume, ambao wamekuwa wakifanya hayo baada ya kufikisha miaka 40 mwaka huu.

Aidha msanii huyo amesema kwamba amezoea kuitwa sura mbaya na kwamba wanapaswa kutafuta maneno mengine ya kumuita.

Pia amesema inaonekana kwamba yeye ni mrembo kuliko wapenzi wao wa miaka 20.

"Sasa kuitwa mazee na sura Mbaya nishazoea munaweza mukatafuta maneno makali mengine yakuniita na wengi wao uwa wanaume mybe I look much better at 40 kushinda your galfriend mwenye ako 25.hatukatai uzee uzee ni sunna ni hatizeeki kizembe hatujitupi wall yangu ikikusinya ni block," Amesema Nyota.

 

 

View Comments