Rudeboy na Mr. P wako tayari kutumbuiza mashabiki wao nchini Kenya
•Peter na Paul walikuwa na nguvu kubwa katika tasnia ya muziki ya Nigeria kabla ya kutengana mnamo 2017.
•Hatimaye madungu hao walisameheana tarehe 17 Novemba 2021.
Wanamuziki wawili mashuhuri Peter na Paul Okoye, wanaofahamika kwa jina lao la awali Psquare, wametangaza mipango ya kutumbuiza nchini Kenya.
Katika video ya instagram kwa akaonti ya Rudeboy, waimbaji ya kibao cha 'Do Me' walitangaza kuwa wanaanza ziara katika miji 100 duniani kote, Afrika Mashariki ikiwemo Kenya, Tanzania, na London kati ya nchi nyingine.
''Unajua nini,ni wakati wa Psquare na tutazuru miji 100 duniani kote,Kenya, Tanzania Afrika Mashariki kote, London, United States. Zitaje,nyimbo mbili mpya zinakuja '' Psquare walisema.
Psquare, ambao sasa wanajitambulisha kuwa Rudeboy na Bw. P baada ya kutengana kwa muda mfupi.
Watakuwa kwenye ziara yao ya kwanza nchini Kenya tangu maridhiano yao mwishoni mwa mwaka jana.
Ndugu hawa Peter na Paul walikuwa na nguvu kubwa katika tasnia ya muziki ya Nigeria kabla ya kutengana mnamo 2017.
Peter aliamua kuitwa Mr. P huku Paul akijitambulisha kwa jina la Rudeboy huku wakitumbuiza mashabiki wao kwa kiwango cha juu sana wakati huo wa utengano.
Hatimaye madungu hao walisameheana tarehe 17 Novemba 2021,na kumbatiana hadharani huko Lagos.
Mke wa Peter na kaka mkubwa wa wawili hao, Jude Okoye walikuwepo na kukumbatiana pia.
Mnamo 2001, "P-Square" ilishinda shindano la "Grab Da Mic", kutokana na hayo Benson na Hedges walifadhili albamu yao ya kwanza, iliyoitwa Last Nite.
P-Square pia waliteuliwa kama "Most Promising African Group" katika Tuzo za Kora miezi mitatu baada ya kutolewa kwa albamu yao ya kwanza. Hatimaye walishinda Tuzo la Amen la 2003 la "Kikundi Bora cha R&B".