In Summary

•Staa wa muziki wa Bongo Fleva na CEO wa lebo ya @kingsmusicrecords @officialalikiba ametangaza rasmi tour yake ya nchini Marekani.

Alikiba
Image: Instagram

Staa wa muziki wa Bongo Fleva na CEO wa lebo ya @kingsmusicrecords @officialalikiba ametangaza rasmi tour yake ya nchini Marekani.

Akieleza kwenye Instagram yake @officialalikiba ameeleza kuwa huu ni mwaka wa nne hajawahi kufanya show Marekani hivyo hiyo inaonyesha ni namna gani ame miss kufanya show katika yaifa hilo.

Ameongeza kuwa Tour hiyo itakuwa maalumu kwa ajili ya album yake ya Only one King.

''Siwezi kusubiri kusherekea nanyi tena mashabiki wangu wapendwa'' Alikiba alisema.

Mwimbaji huyo alisema kuwa  ziara hiyo itaanza Septemba mwaka huu na tarehe  rasmi ya ziara hiyo  itatangazwa hivi karibuni.

Tukio kama hii  lilionwa kwa  Diamond na Harmonize  ambao walishafanya ziara yao Marekani, sasa  imekuwa kama desturi Wasanii kutoka Bongo kufanya ziara hizo  mara kwa mara Merekani. 

Wengi wamedai kuwa ziara ya Alikiba Merekani ni kama chanzo cha kujipima ubabe wake huko Merekani kama walivyoshafanya Diamond na Harmonize.

Alikiba Mwaka  huu anatazamiwa kufanya makubwa sana katika usani wake huko Marekani kulingana na maandalizi yake mazuri yanayoonekana wazi.

Baadhi ya mashabiki wake kutoka Bongo walifurahishwa na uamuzi wa Alikiba kuzuru Marekani  na kuwakilisha muziki wakibongo duniani.

Msanii huyo kando na kuimba, ako na tarjiba ya juu katika kucheza soka, haya yamedhihirika wazi katika baaddhi za mchwano ambazo ameshiriki na timu yake kuibuka mshindi.

 

 

View Comments