In Summary

• Saudi Msosi alisema uwezo wake wa kula mbuzi mzima na wali kilo mbili ulifanya bibiye kumtoroka.

Saudi Msosi- Mshindi wa mashindano ya Tonge la Nyama
Image: Youtube

Mwanamume mmoja kutoka Tanzania aliwashangaza wengi kutokana na uwezo wake wa kula kilo 2 za wali na mbuzi mzima kwa wakati mmoja. Jambo lililofanya mkewe kumtoroka kwa uwezo wake wa kula zaidi.

Jamaa huyu anayejulikana kama Saudi Msosi aliwaacha raia nchi hiyo wakinong'onezana baada ya kushinda shindano liitwalo Tonge la nyama mjini Morogoro baada ya kumaliza donati 40 ndani ya dakika 20 pekee.

Jamaa huyu akifanyiwa mahojiano na mwanahabari mmoja maarufu jimbo hilo, Msosi alisema uwezo wake wa kula zaidi ni kwa sababu aliwahi kutembelea daktari. Daktari aliyempasulia mbarika kwamba ana tumbo kubwa sana tofauti na watu wa kawaida na anatakiwa aendelee kula zaidi.

"Nimetoka tu kula donuts 40 kwa dakika 20. Nilianza kula sahani tatu hadi nne hadi nilipofika ngazi za juu,” alisema Msosi.

"Nilikwenda kuangaliwa na niliambiwa tumbo langu ni kubwa sana," Jamaa aliongeza.

Jambo lililomkosesha amani ni  wakati mkewe alipomtoroka kutokana na anavyokula,na pia alichoka kupika chakula kingi. Aliarifu kwamba nyumbani kwake anakula kila 3 za wali na kuku wawili kwa mlo mmoja, kila siku.

“Mimi ni ''bachelor'', huwa naajiri tu wanawake wanipikie, kisha nawalipa pesa. Kwa sasa nipo ''single,” alisema Msosi.

''Kwa sasa, anaweza kula kilo 10 za wali na mbuzi mzima katika mlo mmoja.''  Jamaa alisisitiza.

Licha ya hayo Msosi mwenye kilo 72 alitaka kukanusha madai kwamba hua hatumii uchawi kushinda mashindano hayo.

Masindano haya adimu anasema kwake yaligeuka kuwa riziki yake.


View Comments