In Summary

• "Kwa hivyo tulimhamisha tu chini ya mto,” Holston alieleza.

Mchezaji wa soka wa zamani taifa la Marekani Mike Holston amezua mjadala mkali kwenye mitandao ya kijamii kuhusu usalama wa watu katika mazingira ya nyoka baada ya video kumuonesha anapambana jino na ukucha na nyoka mkubwa aina ya chatu.

Katika video ambayo ilipakiwa mitandaoni, Holston anaonekana akimrukia chatu huyo kama kipunga na kumnasa kichwani huku wakipambana naye kweli kweli kwa kujaribu kujinasua ila nguvu za Holston zinamzidia.

Video hiyo ilipakiwa katika ukurasa kwa jina Complex na mchezaji huyo wa zamani alielekea pale na kuachia maelezo ni kwa nini alikuwa anang’ang’ana na nyoka huyo huku akidokeza kwamab alikuwa anafanya jaribio la kumusuru kutoka kwa wafanyikazi ambao bure wangegeuza kitoweo.

“Huyu nyoka yuko eneo la kazi na wale watu wa nyuma wangemla, tulipigiwa simu ya kumuhamisha.Ni kawaida sana kuwaona nyoka wa kila aina karibu na maeneo ya Borneo wakitafuta riziki yao ya kila siku, lakini huyu nyoka mkubwa angegeuzwa mlo mtamu kwa Kijiji cha mtaa huu! Kwa hivyo tulimhamisha tu chini ya mto,” Holston alieleza.

Watu walistaajabishwa na ujasiri wa mchezaji huyo mwenye mapande sita huku baadhi wakiamwambia asingeng’ang’ana kumnusuru chatu huyo na badala yake angewaachia watu wamgeuze msosi.

“Kwanini usiwaache tu wale? Kwa nini kijiji cha mtaa kina mlo mbaya? Je, unaweza kuhamisha chakula cha simba? Ni ujasiri na uokozi tata wa wanadamu wakati mwingine kwangu unanishangaza,” shabiki mmoja aliteta.

“Anajaribu kumzuia kupumua tu, akini kwa maelezo ya pembeni kwanini unaweka hapa nyoka ukimkaba koo, sasa iweje mtu akiingia ndani ya nyumba yako na kuanza kukukwida tu?” mwingine alionesha kutoridhishwa kwake na kitendo kile.

Wengine walishindwa kuelewa ilikuwaje alipomwachilia chatu huyo mwisho wa siku huku utani ukizuka kwamba huenda anamshikilia kichwa mpaka sasa hivi kwa sababu kutokana na hasira yule nyoka alionesha, angeachiliwa lazima angemdhuru mtu.

“Wengine wanasema bado anashikilia nyoka hadi leo,” mwingine alipasua kicheko cha utani.

View Comments