In Summary
  • Eric Omondi,Bahati,na Avril wapeana maneno makali kwenye mitandao ya kijamii bada ya Eric kuwatusi wasanii
  • Mchekeshaji huyo alisema kwamba ni wakati wa wachekeshaji kuongoa tasnia ya burudani
Eric Omondi

Mfalme wa ucheshi Eric Omondi atafanya chochote na lolote ili avume kwenye mitandao ya kijamii au kwa kimombo tuseme awe 'Talk of the town'.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram 'aliwatusi' wasanii huku akisema kwamba hamna kitu ambacho wanafanya kwa maana video yake imekuwa ikivuma kwenye mitandao ya youtube kwa siku tano.

"Onyo kwa wasanii wote sisi wacheshi tumechukua usukani, sasa tumethibiti, tutaongoza mkitufuata 

 

Video yangu imekuwa ikivuma nambari moja kwa siku tano sasa, na hili litakuwa hivyo maishani

eric-omondi

Naona @bahatikenya aki STRAGOOO hapo chini yangu at number 2 anajaribu kuingia number one but nampiga tu MANGOTOOO...Sioni @khaligraph_jones anywhere on the whole trending list ni MDOMO tu mingi...@sautisol nikama walioa wote @willy.paul.msafi nitafute niku advise bro...@ringtoneapoko ni Chokoraa man'gaa, Msanii chapashtua POKO Chairman ya MALAYA wote Kenya. I am calling upon all COMEDIANS to rise up...IT IS OUR TIME!!! WE ARE RUNNING THIS CITY!!!" Aliandika Omondi.

Baada ya ujumbe wake uliibua gumzo na hisia tofauti huku msanii Avril akimpa bonge la jibu na kumwambia,

"Mradi hauhifadhi utani na ucheshi mmoja kila wakati hatuna shida ukivuma." Avril Alisema.

avril

Mchekeshaji huyo alionekana kukerwa na usemi wake Avril na kumwambia kuwa,

"Huyu ni nani nilikuwa nazungumza na wasanii sio wanamuziki wa zamani." 

Bahati naye alikuwa na haya ya kusema kuhusu ujumbe wake Eric kuhusu wasanii;

 

"Bro Hio Kufura Umefura isikudanganye Mimi Naeza Kufanya Mbaya Sana Usini Confuse na Ezekiel Mutua!!! Fala Sana 😂😂😂."

bAHATI 1
 
View Comments