In Summary
  • Mwanamume asimulia jinsi alimpata mpenzi wake na mwanamume mwingine siku ya valentines

Siku ya wapendanao wengi huwa wannachwa na wapenzi wao huku mapenzi ya wengine yakinoga kila siku.

Mwanamume mmoja aliwaacha wapangaji wenzake midomo wazi baada ya kusimulia insi alimpata mkewe na mwanamume mwingine kwenye kitanda chao siku ya Valentnes mwaka huu.

"Mimi ni dereva wa malori ya masafa marefu, mpenzi wangu alinipigia simu na kuniuliza kama nitakuwa na nafasi ambapo nilimuambia hapana

 
 

Nilikuwa nataka kumshangaza yaani 'kumsurprise' siku ya valentines, lakini nilipofika kwake nilimpata na mwanamume mwingine wakifanya mapenzi

Tulikuwa katika uhusiano kwa muda wa miaka 5, tayari nilikuwa nasikia kwamba si mwanamke mwaminifu lakini upendo wangu kwake ulinifunga macho

Nilikuwa tayari kumfanya mke wangu, lakini sasa nimefunguka macho nimekuwa nampa kila kitu hata kumtumia pesa lakini kwani alikuwa anachezea hisia zangu," Alieleza Mwanamume.

Je ni jambo lipi ulitendewa na mpenzi wako ambalo hutawahi sahau?

 

 

 

 

 

 

View Comments