In Summary
  • Ata saidika vipi, kama yeye mwenyewe hawezi jisaidia baada ya kupata msaada?ni swali au maswali ambayo wanamitandao na wakenya wamejaza akilini
  • Licha ya muigizaji huyo kupata msaada wa pesa na chakula aliendelea kuwa mraibu wa pombe

Ata saidika vipi, kama yeye mwenyewe hawezi jisaidia baada ya kupata msaada?ni swali au maswali ambayo wanamitandao na wakenya wamejaza akilini.

Hii ni baada ya muigizaji Omosh kusaidiwa na mwihowe kuwasikitisha waliomsaidia kwa kuomba msaada tena.

Licha ya muigizaji huyo kupata msaada wa pesa na chakula aliendelea kuwa mraibu wa pombe.

Wasanii wenzake ikiwemo waliokuwa wanaigiza naye katika kipindi cha Tahidi High wameeleza kuwa Omosh ni mraibu wa pombe na juhudi za kurekebisha tabia zake hazijafua dafu kufikia sasa.

Wanamitandao wameendelea kuashiria ghadhabu na Omosh kufuatia kufichuka kwa video hiyo huku wengi wakipendekeza apelekwe katika kituo cha kurekebisha mienendo ili aweze kupambana na uraibu wa pombe.

OMosh amekuwa akivuma baada ya kuwa kwenye mahojiano na kuomba msaada yena, huku msanii B Classic akijitokeza na kumsaidia muigiaji huyo.

Wakenya tu hawajagadhabihswa na jinsi Omosh anaomba msaada bali jinsi amekuwa akilewa baada ya kupokea msaada.

Upande mmoa wa wanamitandao wamemtania na kusema kwamba wanatiwwa nguvu na jinsi wanajua wanaamka asubuhi wanajifanyia kazi na wanamfanyanyia Omosh.

Ni kitendo ambacho kimezua gumzo mitandaoni na haya hapa maoni ya wanamitandao;

21 Savic; Whenever I feel unmotivated I remember I’m working for sth bigger than me. I’m working for Omosh as well. I can’t slack. Gotta get this bread for the both of us Red heart

KOT OCS: Ama Omosh apelekwe Children home! It can help

Trending in kenya: Hustle hard remember Omosh needs your help.

Katubae, Duchess of Perklands: Words of affirmation and slow strokes is the only way to make this weather bearable. But here we are… trying to get Omosh that tripod

Baada ya video hiyo kuibuka Omosh hajitokeza na kubainisha kama video hiyo ni ya kabla ya kupata msaada au baada ya kupata msaada kutoka kwa wakenya.

Awali akiwa kwenye mahojiano na radiojambo Muigizaji huyo alisema kwamba aliacha pombe baada ya kupata jeraha usoni mwake.

View Comments