In Summary
  • Jemutai atoa sababu ya kumrudia na kumsamehe Hamo
  • Hii ni baada ya mmoja wa mashabiki wake kumuuliza kama alimsamehe Hamo
Jemutai & Hamo
Image: Instagram// Jemutai

Licha ya changamoto zilizokumba mapenzi yao miezi michache iliyopita wacheshi Profesa Hamo na Jemutai wameendelea kupiga hatua kubwakubwa katika juhudi za kuimarisha ndoa yao.

Wawili hao wamezidi kufichua mambo kadha wa kadha, huku kupitia kwenye mitandaoya kijamii ya youtube Je mutai akifichua sababu ya kumsamehe Hamo.

Hii ni baada ya mmoja wa mashabiki wake kumuuliza kama alimsamehe Hamo.

"Ndio nilimsamhe Hamo baada ya kugundua sisi sote tumekosa, na baada ya mazungumzo, hakuna mtu ambaye ni kamili ndio maana nilimrudia na hakuna mwanamke angependa kuona watoto wake wakiteseka,"

Pia mwingine aliuliza kwanini mchekeshaji Hamo amekuwa akimficha mke wake, na alikuwa na haya ya kusema;

"Mke wangu hapendi mambo ya mitandao ya kijamii sana, sijamficha, lakini kila kitu tunafanya miatndaoni huwa tunamwambia,"

View Comments