In Summary

•Mulamwah ambaye pia ni muuguzi alisema kwamba bintiye alipigwa picha zaidi ya kumi na wazungu wenye taaluma kubwa ya upigaji picha.

•Mulamwah alisema kwamba aliamua kufungulia mtoto wake kurasa za mitandao ya kijamii ili zije kumsaidia baadae.

Image: INSTAGRAM// MULAMWAH

Mchekeshaji David Oyando almaarufu kama Mulamwah amefichua kuwa picha za binti yake ambazo alionyesha hadharani kwa mara ya kwanza siku ya Jumatatu zilikuwa ghali mno.

Akiwa kwenye mahojiano na Mungai Eve, baba huyo wa mtoto mmoja  aliweka wazi kwamba picha moja tu ilimgharimu shilingi elfu sita.

Mulamwah ambaye pia ni muuguzi alisema kwamba bintiye alipigwa picha zaidi ya kumi na wazungu wenye taaluma kubwa ya upigaji picha.

"Niliona ni poa niweke picha watu wamuone. Picha zilipigwa kitambo, ziko nyingi zaidi ya kumi. Zilipigwa na wataalamu, wazungu fulani hapo. Picha moja ni elfu sita" Mulamwah alisema.

Alieleza kuwa aliamua kutafuta huduma za wataalamu wa kupiga picha ili binti yake atakapokuwa mkubwa awe na picha nzuri za kumbukumbu.

"Lazima upate picha nzuri yenye hata unaweza weka kwa ukuta wa chumba cha malazi. Ni vizuri hata yeye akikua awe na picha nzuri za kumbukumbu. Atapata picha zake na video nyingi, kuna barua pepe yake ambapo huwa tunamuwekea vitu zake kubwa. Akiwa mkubwa tutampatia namba ya siri afungue aone" Alieleza Mulamwah.

Mulamwah alisema kwamba aliamua kufungulia mtoto wake kurasa za mitandao ya kijamii ili zije kumsaidia baadae.

"Naamini siku moja itakuwa ya manufaa kwake, hata kama sio saa hii. Wengi huko nje wanasema eti mitandao ya kijamii haileti pesa..sisi wenye tuko tunajua manufaa yake. Nafahamu umuhimu wa  mtoto kuwa na kurasa za mitandao  ya kijamii" Mulamwah alisema.

Siku ya Jumatatu msanii huyo mwenye umri wa miaka 28 alifichua sura ya bintiye aliyezaliwa mwezi mmoja uliopita kwa mara ya kwanza.

Aliendelea kuahidi kumpatia maslahi ya bintiye kipaumbele kila wakati huku akimtakia maisha marefu na  baraka tele maishani.

"Malkia mwenyewe @keilah_oyando. Leo mniruhusu niringe na kifurushi changu cha furaha. Maneno hayawezi eleza jinsi alivyo mrembo. Maisha yangu yalibadilika punde ulipowasili. Maslahi yako yatakuwa ya kwanza kila wakati. Nakutakia maisha marefu na mafanikio. Asante @carrol_sonie kwa zawadi hii nzuri. Nawapenda nyote. Baraka." Mulamwah aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram.

View Comments