In Summary

•Omondi  amemjibu zuchu ambaye alikuwa anapuzilia mbali maneno ya muigizaji huyo, huku akisema wanamuziki wa Tanzania wameamua kuwa na mtindo mpya ambao utawasaidia kujulikana   nje ya eneo lao

erick omondi
Image: Hisani

Mchekeshaji Erick Omondi  jumanne amejitokeza na kutetea kauli yake kwamba muziki wa bongo flavour ambao umefanya waimbaji wengi wa Tanzania wavume ameanza kupotea.

Kupitia mtandao wake wa Instagram, Omondi  amemjibu zuchu ambaye alikuwa anapuzilia mbali maneno ya muigizaji huyo, huku akisema wanamuziki wa Tanzania wameamua kuwa na mtindo mpya ambao utawasaidia kujulikana   nje ya eneo lao.

"Bongo flavour haiwezi kufa. wasanii wanatoka nje ya eneo lao,  kutafuta  utofauti wa kujaribu sauti mpya.  haijawahi shuhudiwa  kuua tasnia yoyote, tasnia ya muziki ni kubwa sana,  wacha msanii ajaribu mambo yao. Hayo ni mabadiliko" Zuchu alisema 

Kufuatia kauli hio Eric Omondi amejitokeza na kutetea kauli yake huku akimjibu staa za huyo wa Bongo na kumweleza kwamba wanamuziki wa Kenya walianza hivyo na mziki wao ukapotea

"Dada yangu mpendwa,  hivi ndivyo inavyoanza, huwa tunaanza kwa kupoteza uhalisia na utambulisho wetu na kutoa visingizio vyake.Huku Kenya tulianza vivyo hivyo na Muziki wetu ukapotea" Omondi alisema

Aliendelea kueleza madhara ambayo yanaweza sababishwa na mtindo wa Amapiano na kusema mtindo huo ni kama Basi ambalo linapita na kuwaonya wasipojichunga linaweza kuwabeba na mtindo wao kusahaulika.

"Bongo flavour iko SAWAA kabisa na hakuna haja ya kuwaacha Bongo Fleva ati kwa ajili ya 'diversify' Amapiano ni Basi tu linapita ila sisi tundapanda bila kujua linaenda wapi, tutashindwa kurudi nyumbani.tutakuwa tunauza sera zao na kushindwa kurundi nyumbani. tutakuwa tunauza tamaduni zao na kuua zetu za nyumbani" Mchekeshaji  Omondi alinakiri

Isitoshe alipongeza Zuchu kwa wimbo alioimba wa 'Sukari' ambao uliwavutia sana kwa mdundo wa wake na pia sauti nyororo iliyoimba.

"Unapoimba 'Sukari' kwa sauti hiyo tamu ya kweli ya bongo na mdundo . unachofanya kimsingi ni kuinua na taifa na Bendera ya Tanzania"

View Comments