In Summary
  • Mgombea Useneta wa Nairobi Karen Nyamu hana radhi kuhusu kusema 'Ruto ni chuma imesimama'
Karen Nyamu akihutubia wafanyibiashara wadogo kutoka kaunti ya Nairobi katika makao ya naibu rais William Ruto mapema mwezi Desemba.
Image: INSTAGRAM// KAREN NYAMU

Mgombea Useneta wa Nairobi Karen Nyamu hana radhi kuhusu kusema 'Ruto ni chuma imesimama'.

Wakati wa mkutano wa kampeni wa William Ruto jijini Nairobi, Karen alimwita Ruto kama 'Chuma imesimama' na 'Warembo kama yeye'.

Matamshi hayo yalizua kizaazaa kwenye mitandao ya kijamii, huku wanamtandao wakimkashifu Karen Nyamu kwa kutumia lugha chafu katika mkutano huo.

Akizungumza na mpasho Karen alifafanua alichokuwa anamaanisha na matamshi yake.

Katika mahojiano ya kipekee, alisema hatamtumbuiza Raila Odinga 'mzee' anayelazimishwa kwa Wakenya.

“Nilichomaanisha ni kwamba kuna watu wanakaa hotelini na kutuchagulia mgombea urais...hawa Mt Kenya Foundation wanataka tumchague Raila, kuna watu hawafuatilii siasa kwa hiyo nikizungumzia vyumba vya hoteli wanadhani. ya ngono."

Hoja yangu ilikuwa huwezi kukaa hotelini...mchague mgombea urais ambaye sisi (Warembo) tunaona ni mzee ... lakini tuko na kitu kimesimama hapa...mtu kijana, mwenye nguvu," Karen alisema.

Mama huyo  alisema haombi radhi na maoni hayo, na bado angemtaja Ruto kama 'Chuma imesimama'.

"Pamoja na kwamba ilikuwa dhana ya ngono, hoja ilikuwa 'Raila ni chuma mzee Ruto ni chuma imesimama'. Ninaweza kurudia hivyo tena na tena."

Katika mkutano huo, Karen Nyamu alisema kuwa wanawake wako nyuma ya William Ruto.

"Nimetumwa na warembo wote wa nchi hii, wanasema wanatupangia mzee pale kwa hoteli wawache madhara bana. Sisi tuko na chuma hapa, tunataka chuma ile imesimama...mnataka Chuma ya kusimamishwa kazi?" Karen Nyamu aliuliza.

 

 

 

 

View Comments