In Summary

• Alisema kuoa msichana  mrembo ni sawa na kurusha mawe kituo cha polisi na hivyo ni jambo la busara kuchagua wale ambao si warembo sana.

• Aliwashauri viijana kuoa  rika lao kuzuia matatizo yanayoshudiwa kwenye ndoa za siku hizi

Pst James Ng'anga
Image: HISANI

Mhubiri wa Neno Evangelism, James Ng'ang'a  amewaonya wanaume wa Kenya dhidi ya kuoa wanawake ambao ni warembo kupidukia.

Ng'anga alisema kuoa msichana  mrembo ni sawa na kurusha mawe kituo cha polisi na hivyo ni jambo la busara kuchagua wale ambao si warembo sana.

kupitia video ambayo inasambazwa mitandaoni, Ng'ang'a anaonekana akiwapa mafunzo vijana kuhusu vipengele ambavyo mwanamme anafaa   kuangalia wakati anapanga kupata jiko.

"Ni wangapi hawajaolewa? Tafuta ng'ombe kama wewe ambayo inakula nyasi kama wewe muondoke..ukichukua hawa wasichana wadogo wadogo utaachwa ..ata usitake mrembo sana ... ukitafuta mrembo  sana  utangangana na wanaume... tafuta mrembo mwenye urembo wa asilimia 10-15%." alisema Ng'ang'a.

Aliwashauri viijana kuoa  rika lao kuzuia matatizo yanayoshudiwa kwenye ndoa za siku hizi.

"Ushauri  wangu..  tafuta mtu wa rika lako. Usimtafute mrembo sana, la sivyo, utakuwa ukigombana kila siku"

View Comments