In Summary
  • Akothee ni gwiji maarufu wa mitandao ya kijamii na msanii mkubwa wa muziki ambaye amekuwa katika tasnia ya burudani kwa muda mrefu
  • Anafanya kazi yake ya muziki kwa kutoa vibao vya kupendeza na vya hali ya juu
Esther Akoth

Akothee ni gwiji maarufu wa mitandao ya kijamii na msanii mkubwa wa muziki ambaye amekuwa katika tasnia ya burudani kwa muda mrefu.

Anafanya kazi yake ya muziki kwa kutoa vibao vya kupendeza na vya hali ya juu.

 Kando na muziki, Akothee anafanya mafunzo ya upishi ambayo anapakia kwenye chaneli yake ya YouTube na ukurasa wa Instagram akiwaonyesha mashabiki jinsi ya kuandaa milo tamu.

Kupitia kwenye insta stories msanii huyo alipakia video akiwaonyesha mashabiki wwake jinsi nyumba yake ilivyoa nyakati za asubuhi, na bila shaka kutokana na picha hizo Akothee anaishi wenye nyumba ya kifahari.

Mbali na maisha yake Akothee amekuwa akiwasaidia watu maskini nchini au wasiojiweza ili kujikimu katika maisha yao.

Akothee anasema hakuna mwanamume anayeweza kumudu kulipa bili zake hata kwa wiki moja. Ikiwa kuna mwanamume yeyote wa Kiafrika anayeweza kumudu basi ajitokeze.

"Hakuna mwanamume mwafrika anaweza kumudu kulipa bili zangu hata kwa wiki moja na kama wewe iko sema," Aliandika Akothee.

Haya basi wanaume mmepewa nafasi nzuri, ama mnaniambia niwache kuwaamshia ulcers.

 

View Comments