In Summary
  • Risper Faith aapa kuwa mwaminifu kwa mumewe hadi mwisho
Image: Risper Faith/INSTAGRAM

Aliyekuwa sosholaiti Risper Faith ameapa kuwa mwaminifu kwa mumewe hadi mwisho. Haya yanajiri siku moja baada ya wanandoa hao kusherehekea mwaka wao wa tano wa ndoa.

Risper Faith na Brian wamefanikiwa kubaki pamoja licha ya changamoto nyingi.

Kupitia chapisho lake, Risper alifichua kuwa walikuwa wamevumilia misukosuko mingi.

Faith alidai kwamba wengi waliamini kwamba ndoa yao haitadumu.

Alisema kuwa baadhi ya watu walifikia hatua ya kubahatisha kwamba wangetengana baada ya wiki moja pekee. Hata hivyo, wameweza kukaa kwa muda mrefu.

"Safari yetu si kamilifu. Lakini ni yetu, na nitabaki nawe hadi mwisho...nakupenda," Aliandika Faith.

Ndoa za wakati uu wa sasa hazidumu kwani baadhi ya wenzi hawataki kupitia changamoto tofauti kama wanandoa licha yao wanagura na kuanza kuishi maisha yao peke yao.

Hii ndio sababu kuu kumekuwa na asilimia kubwa ya 'baby daddie' na baby mamas' nchini.

 

 

 

 

View Comments