In Summary

•Ametangaza kujitosa  kwenye kinyanganyiro cha Urais amesema wakati umefika  waondoe dhana mbaya kuhusu upaazi wa mmea wa bangi

•Alitaja endapo akachaguliwa rais atahalalisha mmea  wa bangi na kuanzisha ukulima wake jambo ambalo litasaidia vijana wengi kupata ajira

George Wajackoya
Image: HISANI

Wakili George Wajackoya ameahidi kuhalamisha bangi endapo Wakenya watampigia kura kuwa rais kwenye uchaguzi mkuu ujao, Agosti 2022.

Wakili huyo ambaye ametangaza kujitosa  kwenye kinyanganyiro cha Urais amesema wakati umefika  wakenya waondoe dhana mbaya kuhusu upanzi wa mmea wa bangi.

Vilevile alitaja endapo akachaguliwa rais atahalalisha mmea  wa bangi na kuanzisha ukulima wake jambo ambalo litasaidia vijana wengi kupata ajira.

Alieleza kuwa matumizi ya bangi ni sawa na  yana manufaa tele kwa afya.

"Sisi kazi yetu itakuwa kupanda bangi kisha kuuzia wale wavutaji wa nchi za nje,alafu  tunapata hela ambazo zitasaidia  kujenga nchi yetu" alisema Wajackoya.

Aliendelea kueleza kwamba wakati umefika viongozi na wananchi wamalize dhana potovu kuhusu Bangi  huku akihoji uhalalisha wa sigara ilhali pia  zinamadhara mengi.

"sisi ndio wajinga, tulipumbazwa na dini.. halafu tunaambiwa hii ni mbaya, Chang'aa ni mbaya, bangi ni mbaya lakini Whiskey na sigara ni nzuri kwa sababu zinatoka nchi za nje," alisema. 

 

 

View Comments