In Summary

• Rapa Drake ameacha kuwafuata Rihanna na  A$ap ambao walitangaza kuwa  wanatarajia mtoto wao wa kwanza  mwaka huu 2022

• Drake  ambaye alikuwa mpenzi wa zamani wa Rihanna ame - unfollow wapenzi hao

 

Rapa Drapa
Image: hisani

Rapa Drake ameacha kuwafuatialia Rihanna na  A$ap kwa Instagram ambao walitangaza kuwa  wanatarajia mtoto wao wa kwanza  mwaka huu 2022.

Drake  ambaye alikuwa mpenzi wa zamani wa Rihanna ame - unfollow wapenzi hao huku wanamitandao wakianza tetesi kwamba amekerwa na Rihanna kuwa na mimba ya A$ap.

Jumatatu Rihanna na mpenzi wake walitangaza hadharani kuwa  wanatarajia kifungua mimba wao na kuonekana wakiwa na furaha isiyokifani.

Habari hizo za ujauzito wa Rihanna zilizogonga vichwa vya habari kwenye majukwaa yote ya habari.

Habari za Rihanna  zimetrendi kwa siku tatu mtawalia pale twitter.

Rihanna ni msanii wa kike  anayefuatiliwa zaidi kwenye mitandao ya kijamii na pia ngoma zake zinasikizwa dunia kote.

 

View Comments