Hisani Mwanamuziki Akothee

Mwanamuziki Esther Akoth almaarufu Akothee amemjibu  Dennis Karuri akisema kwamba hana nguvu kujimbazana kwa mtandao.

Jumatatu, Karuri alisema mwimbaji Akothee ni msumbufu wakati anaporembeshwa ili apigwe picha.

Kupitia ukurasa wa instagram Akothee  amekiri kwamba ameona habari ambazo zinasambazwa kwenye mitandao ya  kijamii na hayuko tayari kujishughulisha na habari hizo kwani ni za kutafuta kiki .

Kulingana naye,Karuri anatafuta kiki kwa mitandao kwa kutumia uongo kumharibia jina  jambo ambalo amesema atalipuuza kwa sababu amebaini njia anayotaka kutumia kujulikana.

"Ninashughulika na afya yangu na jinsi pesa zangu zinavyoweza kunifanyia kazi, sina wakati wa kushughulika na wanaotafuta umaarufu, sina nguvu ya kupigana online ! Naweza kuwa napigana na mchawi, aniregeshe kitandani," alisema Akothee.

Isitoshe, alieleza kuwa hatamchukulia hatua zozote za kisheria na anaendelea kufuatilia afya yake ambayo kila siku inaendelea kuimarika.

"Kula vya kwako  . Hakuna habari. Sitatengeneza chapa ili kuinua chaneli zako, chapisha tu kazi zako na achana na jina langu limpumzike.

View Comments