Kanye West aahidi kumfanya French Montana Bilionea
• Rapa na muigizaji wa Marekani Kanye West amemuahidi rafiki wake wa kitambo French Montana kwamba atamsaidia kwa chochote kile kumfanya awe miongoni mwa mabilionea.
Rapa na muigizaji wa Marekani Kanye West amemuahidi rafikiye wa kitambo French Montana kwamba atamsaidia kwa chochote kile kumfanya awe miongoni mwa mabilionea.
Kupitia ukurusa wa instagram, French Montana alikuwa na furaha isiyo na kifani baada ya kupata ujumbe kutoka kwa msanii huyo sifika wa Marekani.
Montana alipakia picha iliyokuwa ikionyesha mazungumzo baina yake na Kanye West, ambapo Kanye alikuwa akimweleza kuwa atamsaidia kufikia hadhi ya mabilionea.
Ni siku za hivi majuzi wasanii hao wameonekana kwenye studio huku ikitabiriwa kuwa watatoa wimbo utakao kuwa kipenzi cha wengi.
Kwa mujibu wa French Montana wameandaa nyimbo tano ambazo muda wowote wanaweza achilia collabo hizo huku wakiwaomba mashabiki wao wakae tayari.