In Summary

•Mwanamuziki wa Tanzania  Kusah amefunguka mazito baada ya mama wa mtoto wake Ruby  kuzua madai kwamba  alikuwa anatumia ushirikina  wakati walikuwa wakiishi  pamoja.

•Mimi sina mengi ya kuongea kwa sababu sio mara ya kwanza kwake kuongea maneno hayo

Mwanamuziki Kusah
Image: Hisani

Mwanamuziki wa Tanzania  Kusah amefunguka mazito baada ya mama wa mtoto wake Ruby  kuzua madai kwamba  alikuwa anatumia ushirikina  wakati walikuwa wakiishi  pamoja.

Wiki jana, Ruby alieleza yote yaliyokuwa  yakiendelea baina ya wapenzi hao wawili hadi siku ambayo aliamua kutoka kwa ndoa yake.

Ruby ni msanii anayetambulika sana kwa sauti yake nyororo, walikosana na Kusah miaka miwili iliyopita na  mwaka huu ndio aliamua kueleza yalitokea kwenye ndoa.

Kupitia kituo kimoja cha habari nchini humo, Kusah ameeleza kuwa Ruby, siku za hivi  majuzi amekuwa akitumia ukurasa wa instagram kueneza uongo  na kukiri kuwa yote aliyosema amemuachia Mungu.

"Mimi sina mengi ya kuongea kwa sababu sio mara ya kwanza kwake kuongea maneno hayo, tushamalizana ni miaka miwili sasa lakini tumebahatika kupata mtoto, kwa hiyo sisi ni wazazi, lakini ukiona mtu anathubutu kuandika ," alisema Kusah.

Alikana  madai  ya kupeleka Ruby  kwa mganga  huku akisema anayepaswa kujibu madai hayo ni Ruby  na si yeye.

"Mambo ya kumpeleka Ruby kwa Mganga, yeye ndio kusema maneno, kwa hivyo sina mamlaka yakujibu,hata mkimuuliza yeye itakuwa  ni kitu kizuri," alieleza.   

 

View Comments