20 February 2022 1 Min Read
'Niko single,'Corazon Kwamboka atangaza kuachana na baba ya watoto wake
In Summary
- Katika chapisho lingine, alirejelea ujumbe wa kutengana kwa kutumia waridi jeusi linaloashiria kifo, na huzuni
Wakili Corazon Kwamboka kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram amewaambia mashabiki wake kwamba yuko single.
Katika chapisho lingine, alirejelea ujumbe wa kutengana kwa kutumia waridi jeusi linaloashiria kifo, na huzuni.
Corazon aliandika "Niko single, najichagua mwenyewe. Maisha yanaendelea."
Haya yanajiri mwezi mmoja baada ya kusisitiza kwamba ana kila kitu ambacho amewahi kutaka kwa Frankie.
Akimtakia heri ya siku ya kuzaliwa ya 32, Corazon alisema, "Wewe ndiye mwanamume, mkarimu zaidi, mvumilivu ninayemjua. Asante kwa kuwa rafiki yangu bora na mfumo mkuu wa usaidizi."
Wawili hao wamebarikiwa na watoto 2.