In Summary

•Mdee alisema anachukulia uzazi kama baraka na jambo la kipekee ambalo hawezi kujuta kamwe. 

•Rotimi vilevile alisema anafurahia hatua ya kuwa mzazi na anaridhia sana katika kusaidia katika ulezi wa mwanawe.

•Vanessa alieleza kuwa mwanawe Seven Adeoluwa Akinosho ambaye kwa sasa ana umri wa miezi mitano anaendelea kukua vizuri.

Image: INSTAGRAM// VANESSA MDEE

Malkia wa muziki kutoka Tanzania Vanessa Mdee amekiri kuwa anafurahia sana hali yake mpya ya mama.

Akiwa kwenye mahojiano na Lil Ommy, Mdee alisema anachukulia uzazi kama baraka na jambo la kipekee ambalo hawezi kujuta kamwe. 

"Najiskia poa. Kuwa mama ni kitu cha kipekee sana. Natamani mashoga zangu ambao wamewahi kuwa na watoto wangeniambia. Kama wangeniambia kitambo ningesema nakosa kweli, lakini sikuwa naelewa. Ni kitu kigumu kueleza kwa mtu ambaye hajawahi kuwa mama. Imekuwa baraka, nafurahia wakati wote" Mdee lisema.

Mpenzi wake Rotimi vilevile alisema anafurahia hatua ya kuwa mzazi na anaridhia sana katika kusaidia ulezi wa mwanawe.

"Kwangu huo ni wakati wa kupumua na kuwa na familia yangu na kuangazia mambo yangu mazuri ambayo najali zaidi. Borake ananiona na kuona jinsi tulivyo na kusoma kadri iwezekanavyo, huo ni wakati muhimu zaidi kwangu. Ni vizuri kuona akikua kila siku" Rotimi alisema.

Vanessa alieleza kuwa mwanawe Seven Adeoluwa Akinosho ambaye kwa sasa ana umri wa miezi mitano anaendelea kukua vizuri.

Mpenzi huyo wa zamani wa Juma Jux alisema mwanawe amefanya ulezi kuwa rahisi kwao kwa kuwa hawasumbui sana.

"Yeye ni mtoto mzuri. mkarimu, mwerevu. Ni mtaratibu sana, amepata hilo kutoka kwa babake. Halii sana, atalia akiwa na njaa ama amechafua diapers. Akiwa na usingizi analala mwenyewe. Yeye ni jasiri" Mdee alisema.

Mdee na Rotimi walitangaza kuhusu kuzaliwa kwa mtoto wao wa kwanza mnamo mwezi Septemba mwaka jana.

View Comments