'kikundi chetu hakina shida' Mbogi Genje yaeleza
• Kikundi cha Mbogi Genje kimejitokeza na kukanusha madai yaliyoibuliwa na Msanii KRG kwamba wasanii wa kikundi hicho wanahangaika kwa sababu hawana pesa.
• Wasanii hao kwa ghahabu walitoa taarifa kupitia ukurusa wao wa Instagram kueleza kilichokuwa kikiendelea.
Kikundi cha Mbogi Genje kimejitokeza na kukanusha madai yaliyoibuliwa na Msanii KRG kwamba wasanii wa kikundi hicho wanahangaika kwa sababu hawana pesa.
Kutokana kauli hiyo, wasanii wa kundi hilo siku ya Jumatano walipakia video wakionyesha bunda la noti kama lengo la kukana madai yaliyoibuliwa na msanii huyo kuwa hawana hela.
Wasanii hao kwa ghahabu walitoa taarifa kupitia ukurusa wao wa Instagram kueleza kilichokuwa kikiendelea.
“Tuzungumze ukweli Smady tings ni miongoni mwa wasanii bora wa dancehall na anayefanya kazi nyingi zaidi za muziki, bila kumsahau Rudra Kartel kwa sababu wote wanasikika kama Vybz Kartel, ikiwa tutahitaji kuzungumza juu ya wasanii bora wa dancehall nchini, basi wawili ni bora,” walisema.
Vilevile walibaini kuwa vipaji sifika vya muziki humu nchini vinatoka mitaa ya mabanda huku wakieleza nia yao ni kuwakuza vijana zaidi kutoka maeneo hayo.
“Vipaji vingi vinazaliwa na kuishi gheto na ndio maana tunarudi kuwatia moyo vijana wenzetu. Wasanii waache tabia mbaya na wafikirie kusaidia wengine badala ya kujaribu kuwadunisha kwa sababu wanajiona kuwa bora."