Mwimbaji wa Nigeria Yemi Alade ameteuliwa kuwa balozi wa Afrika atakayekuwa miongoni mwa kikundi kitakachokuwa kinahimiza Waafrika kujitokeza kwa wingi ili kupokea chanjo ya kujikinga na virusi vya Corona.
Lengo la kampeni hiyo ni kuhamasisha Waafrika kuhusu umuhimu wa kujitokeza kwa wingi kupokea chanjo dhidi Covid-19.
Yemi atakuwa anazuru nchi mbalimbali za Afrika huku akitoa mwito kwa watu kujitokeza na kuwaeleza umuhimu wa kupokea chanjo.
Yemi alieleza kuwa atatoa wimbo ambao maudhui yake yataangazia kampeni za kuhimiza Waafrika kujitokeza kwa wingi kupokea chanjo ambazo zinapeanwa bila malipo.
"Ninafuraha kuwa sehemu ya #ItsUptoUs, vuguvugu hili linalohimiza Waafrika kuchukua jukumu la kufanya ulimwengu kuwa salama tena. Nina furaha kutoa sauti yangu kwa suala hili muhimu na wakati huu,” alisema Yemi.
Mwaka jana kampeni za kuhimiza Waafrika kujitokeza kwa wiki kuchukua chanjo zilifanyika katika nchi saba,Kenya ikiwa mojawapo ya nchi zilizofaidika na mafunzo hayo