In Summary

•Mfanyabiashara mashuhuri wa matatu Jamal Marlow almaarufu Jimal Rohosafi amefunguka na kueleza kuwa aliwahi kuwa Kondakta  kwa zaidi ya mwaka mmoja.

Jimal Rohosafi
Image: Instagram

Mfanyabiashara mashuhuri wa matatu Jamal Marlow almaarufu Jimal Rohosafi amefunguka na kueleza kuwa aliwaHi kuwa Kondakta  kwa zaidi ya mwaka mmoja.

Mfanyabiashara huyo anayevutia hisia mbalimbali kwenye mtandao wa kijamii amewashauri vijana kujituma bila kujali changamoto wanazokumbana  nazo na kuwa na imani siku za usoni mambo yatakuwa shwari bila shari.

Rohosafi inakadiriwa kuwa ana takribani Matatu  32 ambazo husafirisha watu sehemu mbalimbali  jijini.

Pamoja na utajiri wote huo, Jimal amebaini kuwa bado huwa anatumia matatu kusafiri kwenda sehemu mbalimbali za jiji, kwa kuwa huo ndio mtindo wake wa maisha.

 "Matatu ni sehemu ya maisha yangu, nina Matatus 32. Kila wikendi niko gereji, nikishirikiana na wafanyakazi wangu....ni sehemu ya mapenzi yangu. Ninaishi, ninapumua na kuzungumza Matatu," alisema Jimal.

 Rohosafi ni baba wa watoto watatu ambaye ni mwenyekiti wa Chama cha waendeshaji Matatu na umaarufu wake ulianza katika sekta hiyo ya Matatu.

"Mwaka 2009 nilikuwa Kondakta,2011-2013 nilikuwa dereva. Kisha nikaibukia kumiliki sacco zaidi y 6 na kuwa mwenyekiti wa waendeshaji."

View Comments