In Summary

•Mwanasoshalaiti huyo alisisitiza kuwa kuzaliwa kwa mtoto wake wa kwanza ni jambo ambalo alikuwa amepangia.

Image: INSTAGRAM// VERA SIDIKA

Mwanasoshalaiti Vera Sidika ameapa kutawahi pitisha wembe kichwani mwa binti wake wa pekee  , Asia Brown.

Akishirikisha mashabiki wake katika kipindi cha maswali na majibu kwenye mtandao wa Instagram, Vera alifichua kuwa bintiye bado ana nywele alizozaliwa nazo.

"Sijawahi kunyoa nywele zake, sitawahi!" Vera alijibu shabiki aliyetaka kujua iwapo tayari amezinyoa nywele za Asia.

Mwanasoshalaiti huyo alisisitiza kuwa kuzaliwa kwa mtoto wake wa kwanza ni jambo ambalo alikuwa amepangia.

"Nilingoja wakati sahihi ufike.. na mtu aliye sahihi," Vera alisema kuhusu suala la kusubiri miaka sana kabla ya kupata mtoto wa kwanza.

Vera ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 32 alisema anapanga kupata watoto wengine wawili au watatu zaidi. Alisema anapanga kupata mtoto wake wa pili hivi karibuni.

"Napanga kupata watoto wawili ama watatu zaidi. Mume wangu nami tunapenda watoto.. Mwaka ujao Mungu akipenda," Alisema Vera.

Mwanasoshalaiti huyo pia alieleza kuwa kazi zake za kutumbuiza katika vilabu haijaathiri ndoa yake na uzazi kwa namna yoyote.

View Comments