In Summary

• Irene Uwoya anasema kwamba kila mtu hupata shida ila wengine hawajulikani kama wanapata shida kwa sababu wanaowasaidia hawawatangazi.

IRENE UWOYA
Image: INSTAGRAM

Staa wa Bongo Movie Irene Uwoya anahisi kwamba siku hizi ni ngumu sana upate mtu anayetoa msaada bila kutangaza ama kwa maneno au katika video haswa katika hiki kizazi cha TikTok na WhatsApp ambapo kila tukio linarekodiwa.

Uwoya anasema kwamba kila mtu anahitaji msaada hata wao ambao wanaonekana mastaa na kudhaniwa na wengi kwamba pengine hawawezi kuwa na hitaji la kimsaada kutoka kwa watu wengine.

Ila pia staa huyo alichora tofauti inayojitokeza kati ya watu wanaotoa msaada na kusema kwamba kila mtu kwa sababu moja au nyingine huhitaji msaada lakini kinachofanya wengine wao wasijulikane ni kwa sababu wanawapa msaada hawana hulka ya kutangaza.

Sio kwamba hatupatagi shida ila wanaotusaidia hawatutangazi,” aliandika Uowya kwenye Instagram yake.

Katika kile alionekana kuweka kwenye mizani suala la Aristote kumchamba Wema Sepetu kwamba hana gari, Uwoya alikuwa na maana kwamba kila mtu ana nafasi yake katika maisha na kula watu ambao anawategemea kwa kumsaidia kutatua shida fulani ambazo mwenyewe hawezi kuzitatua.

Aidha wafuasi wake walimtaka afafanue zaidi huku wengine wakichukua kauli hiyo na kuanza kuichambua kwa uelewa wao binafsi.

“Hujawahi saidiwa na Aristote wewe, ungejuta,” aliandika shabiki kwa jina Babykher.

Je, unahisi kusaidia mtu halafu tukio hilo lichukuliwe kwa kamera na baadae kupakiwa kwenye mitandao ni vibaya ama ni haki?

View Comments