In Summary

• Mwanaharakati Malisa GJ ameongea kwa uchungu kuhusu video inayosambazwa mitandaoni ikimuonesha Professor Jay akiwa ICU.

• Anasema mwenye alifanya video hiyo amekosea kisheria na kimaadili na kutaka uchunguzi ufanyike ili achukuliwe hatua.

Professor Jay
Image: Malisa GJ (Facebook)

Mwanaharakati wa haki za kibinadamu nchini Tanzania Malisa GJ amedhihirisha wazi kutofurahishwa kwake na video ya msanii mkongwe wa bongo fleva Profesa Jay akiwa hali mahututi na kusambazwa pakubwa kwenye mitandao ya kijamii.

GJ ameandika Alhamisi kwenye mtandao wake wa Facebook akionyesha ghadhabu zake na kusema kwamba aliyerekodi video hiyo alikiuka pakubwa haki za kimsingi za msanii huyo na pia kuonesha kiwango kikubwa cha kukosa utu.

“Nimeumia sana kuona Prof.Jay amerekodiwa akiwa mahututi na video hiyo kusambazwa mitandaoni. Hiki ni kiwango cha juu cha kukosa utu. Hata kama ni kutafuta pesa si kwa njia hii. Tujifunze kuheshimu utu kuliko fedha. Jiulize angekua baba yako ungemrekodi? Ikumbukwe kupiga picha hospitali bila kibali "maalumu" ni kosa kisheria,” aliandika Malisa GJ kwa ghadhabu kali.

Pia mwanaharakati huyo ambaye pia anajiongea kuwa mhisani mwema alielezea kwamba sheria za Cybercrime a mwaka 2015 haziruhusu mtu kuchukua video ya faragha yam tu asiyejielewa kwa kipindi hicho na kuanza kuisambaza mitandaoni na kusema kwamba mwenye alifanya hivo si tu alikiuka haki zac kimaadili bali kisheria pia.

“KIMAADILI amemkosea Jay, familia yake na amewakosea watanzania. Japo kosa hili halina adhabu lakini linabeba laana kwa mhusika. KISHERIA kupiga picha eneo lisiloruhudiwa na kusambaza mitandaoni ni kinyume na sheria ya makosa ya mtandao ya mwaka 2015,” aliendelea kuandika GJ.

Malisia GJ pia ameurusha mzigo wa lawama za kurekodiwa kwa video hiyo kwa wahudumu wa afya katika hospitali ambapo Jay alikuwa amelazwa na kusema kwamba kati ya makundi matatu ya watu ambao wanaruhusiwa kuona Jay, familia, maafisa wa serikali na wahudumu wa afya humo, asilimia kubwa ni kwamba video hiyo ilifanywa na mhudumu wa afya kwa sababu si rahisi mtu wa familia anaweza fanya hivo wala mtu kutoka serikalini kwani wanaijua sheria na maadili pia.

Kwa kuwa ICU kuna CCTV, nashauri wapitie "footage" wataona ni nani aliyehusika kufanya tukio hili la kinyama. Kama ni mtumishi achukuliwe hatua za kinidhamu na za kisheria. Hatua za kinidhamu ni kama kusimamishwa kazi na kufutiwa leseni kwa kwenda kinyume na kiapo chake cha kulinda siri za mgonjwa. Na hatua za kisheria ni kupandishwa mahakamani na kufunguliwa mashtaka ya kurekodi na kusambaza maudhui yasiyofaa mtandaoni, kinyume na sheria ya makosa ya mitandao ya mwaka 2015. Akipatikana na hatia, namuomba Hakimu asimpe faini au kifungo bali amtandike vyote kwa pamoja. Atumikie miaka mitatu jela na alipe faini isiyopungua 5M kama sheria inavyoeleza. Hii itakua fundisho kwa "vishohia" wengine wanaodhani matatizo ya mtu ni fursa ya wao kuuza habari,” ameshauri Malisa GJ na kumaliza.

View Comments