In Summary

•Vera alisema  ndoa yake imejawa na raha tele na ni ya kusisimua kwani anachumbiana na mtu anayemfaa.

•Jambo lingine ambalo alifichua kuhusu maisha yake ni kuwa kamwe  hajawahi kuajiriwa katika maisha yake.

Image: INSTAGRAM// VERA SIDIKA

Siku ya Jumamosi mwanasoshalaiti Vera Sidika alishirikisha mashabiki wake katika kipindi cha maswali na majibu kwenye ukurasa wake wa Instagram ambapo alijibu maswali kadhaa kuhusiana na maisha yake.

Maswali mengi ambayo yaliibuka ni kuhusu ndoa yake na Brown Mauzo  na vilevile kuhusu binti yake wa pekee Asia Brown.

Katika kipindi hicho, mwanasoshalaiti huyo mwenye umri wa miaka 32 alifichua kwamba alichumbiana na Mauzo kwa kipindi cha miezi sita kabla ya kukubali kupata mtoto naye.

"Miezi sita hasa!" Vera alijibu shabiki aliyetaka kujua muda ambao ilimchukua kukubali mtoto na mumewe.

Vera alisema  ndoa yake imejawa na raha tele na ni ya kusisimua kwani anachumbiana na mtu anayemfaa.

Mama huyo wa mtoto mmoja aliweka wazi kuwa anafurahia hali ya kuwa mama.

"Shukran sana. Napenda kuwa mama" Vera alijibu shabiki aliyempongeza kwa kuwa mama.

Mwanasoshalaiti huyo pia alifichua kuwa hajawahi kubugia kileo chochote tangu alipopata ujauzito mapema mwaka uliopita.

"Sijawahi kunywa. Hata baada ya kujifungua kwa kuwa nanyonyesha," Vera alisema.

Jambo lingine ambalo alifichua kuhusu maisha yake ni kuwa kamwe  hajawahi kuajiriwa katika maisha yake.

View Comments